Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania na Qatar Kushirikiana katika Maendeleo ya Michezo na Uwekezaji.
Feb 16, 2026
Tanzania na Qatar Kushirikiana katika Maendeleo ya Michezo na Uwekezaji.
Mhe. Waziri Paul Makonda akutana na Balozi wa Qatar ambapo amemueleza namna Tanzania inavyoendelea na maandalizi kuelekea Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Paul Makonda amefanya mazungumzo na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Ahmed Abdulla Al-Dossari  kuhusu ushirikiano wa nchi hizo katika uwekezaji kwenye maendeleo ya sekta ya michezo hapa nchini.

Mhe. Waziri Makonda amekutana na Balozi huyo Februari 16, 2026 jijini Dar es Salaam, ambapo alimueleza namna Tanzania inavyoendelea na maandalizi  kuelekea Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 akibainisha fursa za uwekezaji katika miundombinu ikiwemo malazi  jijini Arusha, uboreshaji wa viwanja vya mpira wa miguu, pamoja na kukuza sekta ya utalii.

Alisisitiza umuhimu wa kunufaika na uzoefu wa Qatar uliopatikana wakati wa kuandaa Kombe la Dunia la FIFA 2022, tukio lililotambulika kimataifa kwa ubora wa miundombinu, usimamizi na mchango wake mkubwa katika uchumi na maendeleo ya sekta ya michezo nchini humo.

Vilevile alishukuru nchi hiyo kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania  katika sekta za maendeleo, uwekezaji na diplomasia.

.                  
Kwa upande wake  Balozi Ahmed alisisitiza kuendeleza ushirikiano huo kupitia kubadilishana uzoefu,  kuendeleza miradi ya pamoja itakayochochea maendeleo ya michezo, utamaduni, utalii uwekezaji pamoja  na uchumi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi