Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Makamba Ashiriki Mkutano wa Viongozi wa Dunia wa Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa Afrika
Sep 05, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwenye mkutano wa Viongozi wa Dunia unaojadili Program ya Afrika ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Africa Adaptation Summit) unaofanyika Rotterdam, Uholanzi tarehe 5/9/2022. 

Mkutano huo unalenga kushawishi Washirika wa Maendeleo, Taasisi za Kifedha na Sekta binafsi na marafiki wa Afrika kuchangia fedha kwenye Programu hiyo ya Afrika ambayo inahitaji Dola za Marekani bilioni 25 ifikapo 2025. Benki ya Maendeleo ya Afrika imechangia Dola za Marekani bilioni 12.5.

Mkutano huu unafanyika kama sehemu ya maandalizi ya mkutano wa 27 nchi wananchama wa mkataba wa  mabadiliko ya Tabia Nchi ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba  mwaka huu huko Sharm El  Sheik Misri ambako suala la kuhimili mabadiliko ya Tabianchi kwa Afrika ni moja ya agenda muhimu ya mkutano huo.

Katika Mkutano huo, Waziri wa Nishati amekutana na Viongozi wa Dunia, Wakuu wa Taasisi na Mashirika mbalimbali na kujadiliana nao fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna bora ya Tanzania kunufaika na Mpango huo wa AFRICA ADAPTATION ACCELERATION PROGRAM (AAAP) ambao utaharakisha mipango ya nchi katika kukabiliana na majanga yakiwemo UVIKO-19, ukame, njaa, ajira kwa vijana na mafuriko. 

Mkutano huo uliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Senegal na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika pamoja Mhe. Macky Sally na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kituo cha kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (GCA), Mhe. Ban Ki-Moon.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi