[caption id="attachment_31436" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida (kulia) ofisini kwake mjini Dodoma mapema leo tarehe 09 Mei, 2018.[/caption]
Na. Samwel Mtuwa – Dodoma.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki leo amekutana na balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida mjini Dodoma lengo likiwa ni kujadiliana namna ya kushirikiana kwenye uwekezaji wa madini nchini.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Kairuki alisema lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili maandalizi ya Jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini kati ya Tanzania na Japan.
Alisema kupitia jukwa hilo, wadau kutoka nchi zote mbili watafahamu fursa za uwekezaji katika sekta ya madini kama vile uongezaji thamani ya madini yapatikanayo nchini na namna ya kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo.
[caption id="attachment_31437" align="aligncenter" width="870"]