Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Jenista Mhagama azindua mdahalo wa kitaifa wa kujadili ushirikishwaji wa wananchi katika agenda ya viwanda jijini Dodoma
May 24, 2018
Na Msemaji Mkuu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza wakati wa uzinduzi wa mdahalo wa kitaifa wa kujadili ushirikishwaji wa jamii katika uwekezaji  ndani ya nchi ili kuchangia ajenda ya viwanda uliofanyika leo Jijini Dodoma.Kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tasisi ya Uongozi  Prof Joseph Semboja,Nlanla Gumede kutoka Afrika Kusini na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji  wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tasisi ya Uongozi  Prof Joseph Semboja akizungumza kabla ya kukaribisha mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mdahalo wa kitaifa wa kujadili ushirikishwaji wa jamii katika uwekezaji  ndani ya nchi ili kuchangia ajenda ya viwanda uliofanyika leo Jijini Dodoma..Kulia kwake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama Nlanla Gumede kutoka Afrika Kusini na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo  na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tasisi ya Uongozi  Prof Joseph Semboja wakati wa uzinduzi wa mdahalo wa kitaifa wa kujadili ushirikishwaji wa jamii katika uwekezaji  ndani ya nchi ili kuchangia ajenda ya viwanda uliofanyika leo Jijini Dodoma.

Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji  wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa Akizungumzia umuhimu wa mkakati wa ushirikishwaji wa jamii katika uwekezaji  ndani ya nchi ili kuchangia ajenda ya viwanda uliofanyika leo Jijini Dodoma.

Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji  wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa Akizungumzia umuhimu wa mkakati wa ushirikishwaji wa jamii katika uwekezaji  ndani ya nchi ili kuchangia ajenda ya viwanda uliofanyika leo Jijini Dodoma.

Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji  wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa Akizungumzia umuhimu wa mkakati wa ushirikishwaji wa jamii katika uwekezaji  ndani ya nchi ili kuchangia ajenda ya viwanda uliofanyika leo Jijini Dodoma.

 

 Frank Mvungi-  MAELEZO

Serikali  imewahakikishia Wananchi kuwa itaendelea Kuhakikisha  kuwa wanashiriki Kikamilifu  katika ujenzi wa uchumi wa Viwanda kwa kufungamisha Maendeleo ya Wananchi na ukuaji wa sekta hiyo ili kukuza kipato chao na Kujenga uchumi Jumuishi.

Akizungumza   leo Jijini Dodoma wakati  akifungua  Mdahalo wa siku mbili kuhusu mkakati wa Kuwashirikisha wananchi katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali na Wadau kutoka Sekta binfasi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira  na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na miradi yote inayotekelezwa  hapa nchini na hasa ujenzi wa Viwanda.

 " Kuna umuhimu mkubwa kwa kila mtanzania kushiriki kikamilifu katika dhana hii ambayo Serikali tumeona italeta  tija kwa wananchi kwa kuwashirikisha kikamilifu katika miradi yote mikubwa ikiwemo ule wa Bomba la mafuta , Ujenzi wa reli na ule wa kufua umeme" Alisisitiza Mhagama

Akifafanua amesema kuwa Serikali imebainisha sekta mahususi za kuanzia katika mkakati huo ambazo ni mafuta, gesi, Kilimo na ufugaji, ujenzi na usafirishaji na utalii ambapo mara baada ya kukamilika kwa mkakati huo  tija katika uzalishaji na kukuza uchumi itaongezeka kwa kiwango kikubwa hivyo kuondoa umasikini kutokana na kuwepo kwa uchumi shirikishi.

Aliongeza kuwa kuwepo kwa  mkakati huo kutasaidia kuweka mfumo wa ufuatiliaji na pia kubainisha wadau watakaoshiriki katika kufanya mkakati huo ulete matokeo tarajiwa na hivyo kuzaliwa kwa  Tanzania mpya  kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Pia aliwataka watanzania kuthamini bidha zinazozalishwa hapa nchini ili kusaidia kukuza viwanda vya hapa nchini na kuongeza ajira hali itakayokuza pato la Taifa na mwananchi mmoja mmoja.

 Kwa upande wake Mwenyeki wa Baraza la Uwezeshaji  Wananchi kiuchumi  Dkt. John Jingu amesema kuwa  ili kufanikisha azma ya Serikali kuwezesha wananchi kupitia mkakati huo lazima Serikali ihakikishe kuwa sheria na mikataba yote iwe inakipengele kinacholenga kuwezesha wananchi kwa kuwashirikisha katika miradi ya kisekta  inayotekelezwa.

Pia aliongeza kuwa Lazima makampuni ya  ndani yajengewe uwezo zaidi katika kutoa huduma zenye viwango vinavyotakiwa katika miradi inayotekelezwa hapa nchini.

 Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof.  Joseph Semboja amesema kuwa Taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi katika kuhakikisha kuwa azma ya ujenzi wa uchumi wa viwanda na uwezeshaji wananchi kiuchumi inatimia.

     

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi