Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Hamad Aipigia Debe Zanzibar
May 20, 2017

[caption id="attachment_1348" align="alignnone" width="750"] Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed (kushoto) akimkabaribisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia) wakati alipomtembelea Ofisini kwake mjini Unguja.[/caption]

Na Mwandishi wetu,

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed ameishauri Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuwekeza Zanzibar ili kuwainua kiuchumi wakulima na wavuvi visiwani humo.

Mhe. Hamad amesema Visiwa vya Zanzibar vina maeneo mengi ya uwekezaji  katika kilimo na kwamba uwekezaji mkubwa unahitajika ili kuongeza tija na kukuza uchumi wa Zanzibar.

“Nawahakikishia mkianza kuwekeza katika miradi kama ya mwani, uvuvi na karafuu Benki itapata mafanikio makubwa na kuitumia Zanzibar kama mfano rejea katika utoaji wa mikopo yenye tija nchini,” alisema Mhe.Hamad.

[caption id="attachment_1349" align="alignnone" width="750"] Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed (kulia) akimkaribisha Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Augustino Chacha (wapili kushoto) walipomtembelea Mhe. Waziri Ofisini kwake mjini Unguja. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (wa pili kulia) na Meneja Mikopo wa benki hiyo, Bw. Samuel Mshoto.[/caption] [caption id="attachment_1350" align="alignnone" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akieleza dhima ya Benki hiyo wakati walipomtembelea Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed (wa pili kulia) ofisini kwake.[/caption] [caption id="attachment_1354" align="alignnone" width="750"] Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na Watumishi wa Wizara hiyo.[/caption]

Kwa mujibu wa Mhe. Waziri, Zanzibar ni miongoni mwa visiwa vyenye utajiri mkubwa ambapo ukifanyika uwekezaji wa kimkakati utawanufaisha wananchi wengi visiwani humo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali ilianzisha Benki hiyo ili kusaidia upatikanaji wa mikopo na kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini.

Bw. Assenga ameongeza kuwa Benki inatambua fursa za uwekezaji Visiwani Zanzibar na kuahidi kuanza uwekezaji mkubwa kwa wadau wa sekta za kilimo na uvuvi ambazo ni sekta zinazopewa kipaumbele kupewa mikopo na TADB.

TADB ni taasisi ya kifedha ya serikali iliyo anzishwa kwa ajili ya kutoa mikopo ya fedha ili kuendeleza sekta ya kilimo nchini.

     

Mipangilio
Marekebisho ya Lugha
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi