Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wawekezaji Wazawa Wapewa Rai Kujenga Viwanda vya Dawa
Mar 26, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_29484" align="aligncenter" width="750"] 17. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya magari 181 yatakayokuwa yatayosafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na Mwandushi Wetu, MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa rai kwa wawekezaji wazawa na wafanyabiashara nchini kujenga viwanda vya dawa na vifaa vya tiba hapa nchini ili kuongeza kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda na kukuza ajira.

Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo Jijini Dar es Salaam, kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 yenye thamani ya shilingi bilioni 20.7 ya kusambaza dawa na vifaa vya tiba yaliyotolewa msaada na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD).

“Asilimia 94 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi, hivyo wawekezaji wazawa watumie changamoto hii kama fursa ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa hapa nchini kwetu,” alisema Rais Magufuli.

[caption id="attachment_29478" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa, Laurean Bwanakunu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.[/caption]   [caption id="attachment_29481" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam[/caption]

Rais Magufuli alibainisha kuwa ujenzi wa viwanda hapa nchini utasaidia kuongeza ajira kwa Watanzania hasa vijana pamoja na kupunguza gharama za kuagiza bidhaa nje ya nchi zikiwemo dawa na vifaa vya tiba.

Aidha Rais Magufuli ametoa wito kwa wataalamu na wasomi wazawa wa masuala ya afya na tiba kujiunga pamoja na kuanzisha viwanda vya dawa ili kuchochea uchumi wa viwanda na kuongeza mapato.

“Tunapoteza shilingi bilioni 500 kila mwaka kwa ajili ya kununua dawa nje ya nchi lakini tungekuwa na viwanda vyetu fedha hizo tungetumia kwenye mambo mengine ya maendeleo,” alisisitiza Rais Magufuli.

[caption id="attachment_29482" align="aligncenter" width="750"] Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_29485" align="aligncenter" width="750"] Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari 181 yatakayokuwa yatayosafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam[/caption] [caption id="attachment_29486" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,. Jinsia, Wazee na Watoto akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_29487" align="aligncenter" width="750"] Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishuka katika moja ya magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_29489" align="aligncenter" width="750"] Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mwakilishi Mkazi wa Global Fund, Linden Morrison wakifurahia jambo na wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Madawa (MSD) mara baada ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_29490" align="aligncenter" width="750"] Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikagua baadhi ya magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam. (Picha na:  MAELEZO)[/caption]  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi