Watumishi Ofisi ya Msajili Vyama vya Siasa Wapigwa Msasa Sheria ya Gharama za Uchaguzi
Nov 22, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Baadhi ya washiriki wa mafunzo kuhusu usimamizi wa sheria ya gharama za uchaguzi toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo leo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Mafunzo hayo yanafanyika kufuatia kuwepo kwa uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Amani Zanzibar na Madiwani wa kata 12 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 17 Disemba, 2022.