Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watanzania Milioni 16 Walikuwa Wanafuatlia Ziara ya Rais Tanga Kila Siku
Mar 01, 2025
Watanzania Milioni 16 Walikuwa Wanafuatlia Ziara ya Rais Tanga Kila Siku
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa leo Machi 1, 2025 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ametoa taarifa maalum kwa umma kupitia Waandishi wa Habari kuhusu Ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Tanga na Mkutano wa Tatu wa Nchi Zinazozalisha Kahawa Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu

Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihitimisha ziara yake katika Mkoa wa Tanga leo Machi 1, 2025, tathmini inaonesha kuwa zaidi ya Watanzania milioni 16 walikuwa wakifuatilia ziara hiyo kila siku.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, inaeleza kuwa kwa mujibu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Upimaji Serikalini, Watanzania hao walikuwa wakifuatilia ziara hiyo kila siku kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii.

“Taarifa zetu za thathmini zinainesha kwamba watu waliokuwa wanafuatilia ziara mkoani Tanga kupitia vyombo vya redio na televisheni, kwa sababu sisi sasa hivi tuna kitengo ambacho kinafanya kazi ya kufuatilia ‘viewership,  usikilizaji na usemaji, watu wakiokuwa wakifuatilia ziara mkoani Tanga kila siku walikuwa hawapungui chini ya milioni 16 na wengine wameandika na kusambaza, kwa hiyo  ukijumlisha ni karibu Watanzania wote walikuwa wanafuatilia, hivyo Mheshimiwa Rais anawashukru kwa kufuatilia ziara yake”’ ameeleza Msugwa.

Msigwa ameeleza kuwa ziara ya Mhe. Rais mkoani Tanga imekuwa na mafanikio kwa asilimia 100 kutokana na mahudhurio kuwa makubwa kuliko ilivyotarajiwa ambapo maeneo mengi yaliyoandaliwa yalijaa na watu kukosa sehemu za kukaa.

Msemaji Mkuu wa Serikali ametaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja  Mheshimiwa Rais kutembelea miradi yote kwa asilimia 100 na mingine ambayo haikuwa kwenye ratiba lakini Rais Samia aliitembelea.

“Timu iliyofanya tathmani imeonesha wananchi wamefurahi kwa asilimia zote kwa ziara kufanyika Mkoa wa Tanga, wananchi wa Tanga wamefurahi kwa Mheshimiwa Rais kutembelea miradi inayotekelezwa, wamefurahishwa na maelekezo na ahadi alizotoa na namna ambavyo Serikali imetekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho kinaingoza Serikali”, ameeleza Msemaji Mkuu wa Serikali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi