Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wanaokwamisha Operesheni ya Anwani za Makazi Kuchukuliwa Hatua
Apr 13, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi Wetu - Tanga

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima kuhakikisha anawachukulia hatua wale watakaobainika kukwamisha utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika mkoa huo

Akizungumza hivi karibuni jijini Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi, Waziri Nape ameonesha kutokuridhishwa na kasi ya utekelezaji katika mkoa huo unaoshika nafasi ya pili kutoka mwisho

“Hili la Operesheni ya Anwani za Makazi ni jambo letu sote, tuone shida ya kuwa mkiani, wanaotukwamisha washughulikiwe na kama kuna shida kwenye utekelezaji tuelezane tutatue kwa pamoja”, amezungumza Waziri huyo.

Waziri Nape amesisitiza kuwa uwekaji wa Anwani za Makazi sio zoezi la kawaida ni operesheni maalum iliyotangazwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambapo kukamilika kwake kutarahisisha kufanyika kwa Sensa ya Watu na Makazi na ufikishaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Adam Malima amekiri utekelezaji wa Operesheni hiyo bado haujaanza katika halmashauri tatu za mkoa huo, ambazo ni halmashauri ya Korogwe mji, Korogwe vijijini na Kilindi kutokana na changamoto za kiutendaji

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa Mfumo wa kielektoniki unaoingiza taarifa za wakazi na makazi unafanya kazi vizuri, na Wizara hiyo ipo tayari kutoa wataalamu kwenda kuongeza nguvu kwenye mkoa au halmashauri yeyote ambayo ina uhitaji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi