Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wananchi Kilimanjaro Wampongeza Rais Samia
Mar 09, 2025
Wananchi Kilimanjaro Wampongeza Rais Samia
Sehemu ya wananchi wa Mwanga pamoja na maeneo jirani wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 09 Machi, 2025
Na Mwandishi Wetu

Wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha mkoa huo kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi katika kipindi cha miaka minne.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi maji wa Mwanga-Same-Korogwe, leo Machi 9, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu amesema mkoa huo umepokea zaidi bilioni 900 zilizotumika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Kuhusu mradi wa maji Mwanga Same Korogwe Mhe. Babu amesema wanashukuru kwa kukamilika kwa mradi huo wa maji kwani unaleta mageuzi makubwa katika maisha ya wananchi  wanaonufaika na mradi huo.

"Sisi wana Kilimanjaro tunakupongeza na kukushuruku kwa kutuwezesha na hata pale kulipokuwa na kukawia kidogo tumeona nia yako na kweli tuna kila sababu ya kushukuru kwa makubwa unayotufanyia, kwa sababu fedha zilizokuja mkoani kwetu zimeleta mageuzi makubwa kwenye maisha ya wananchi wetu", alisisitiza Mhe. Babu

Akieleza zaidi, Mhe. Babu amesema kutokana na Mhe. Rais Samia kuuwezesha mkoa huo, wananchi nao wataendelea kumuunga mkono kwa dhati, yeye binafsi na Serikali anayoiongoza ili iendelee kuwapelekea maendeleo zaidi.

Uzinduzi wa mradi wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe umefanyika leo Machi 9, 2024 wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro na umefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi