Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wananchi Kijiji cha Kalenge Waishukuru Serikali Kuwajengea Zahanati
Feb 10, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_50823" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa idara ya tiba Dkt. Grace Magembe akiongea pembeni ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto-Idara kuu Afya Dkt.Zainab Chaula pamoja na wakazi wa kijiji hicho.[/caption]

Na.Catherine Sungura-Uvinza

Wananchi wa Kijiji cha Kalenge wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwajengea zahanati itakayowasaidia kuwaepusha na vifo hasa vitokanavyo na uzazi.

Hayo yamebainishwa jana  na wakazi wa kijiji hicho wakati walipotembelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya  Dkt. Zainab Chaula ambaye ameanza ziara ya usimamizi shirikishi mkoani kigoma ambayo inafanywa na wizara ya afya pamoja na TAMISEMI.

Akiongea kwa furaha bi. Marystela Chishako alisema kuwa wanaishukuru serikali ya Awamu ya Tano kwani kwa kupata zahanati hiyo imewasaidia kupata huduma za afya ikiwemo huduma ya kujifungua ambayo awali walikua wakiifuata kigoma mjini.

[caption id="attachment_50822" align="aligncenter" width="750"] Jengo la kujifungulia ambalo limejengwa katika zahanati hiyo[/caption]

"Tunashukuru kwa serikali hii kutukumbuka Mkoa wa Kigoma,siku za nyuma mama akitaka kujifungua ilibidi aende Kigoma Mjini,ila hivi sasa tunajifungulia hapa hapa kwenye zahanati na tunapata huduma muhimu hapa hapa".

Aidha, alisema zahanati hiyo imewasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto kwani kipindi cha nyuma walikua wakipata matatizo njiani kwa sababu walikua wakisafiri umbali mrefu na kupelekea kupata matatizo wakiwa njiani.

Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Dkt.Chaula aliwahidi kulifanyia kazi ombi lao la kupatiwa kituo cha afya kwani wameshaomba kwa kufuata utaratibu kupitia mkoa.

"Ninawapongeza kwa sababu mmejua umuhimu wa kuwa na kituo cha afya,kwahiyo maombi yataletwa wizara ya afya kutoka TAMISEMI na katika ziara yangu nimeongozana nao hapa na nimepokea ombi hili najua ukitoa ahadi lazima utimize", alisema Dkt. Chaula

Wakazi wa kijiji hicho wametenga eneo la hekari ishiriki,kukusanya mawe pamoja na mchanga kwa kujitolea ili kuweza kujenga kituo cha afya ikiwa ni juhudi za kuiunga mkono serikali kwa kutatua changamoto za huduma za afya karibu na wananchi.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi