Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wananchi Jimbo la Mtera Wanufaika na Mradi wa majisafi ya Bomba
Feb 09, 2020
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_50801" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Maji, mhe. Jumaa Aweso akizungumza kwa furaha wakati akizindua mradi wa maji utakaonufaisha wakazi zaidi ya elfu saba na miatano katika kijiji cha Makang’wa jimbo la Mtera mkoani Dodoma Februari 8, 2020.[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Serikali ya Awamu ya Tano imepongezwa kwa kuwezesha wananchi kufikiwa na huduma ya majisafi na salama baada ya miaka zaidi ya hamsini bila kuwepo kwa huduma hiyo katika eneo lao.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso mwishoni mwa wiki wakati akizindua mradi wa maji katika jijiji cha Makang’a, jimbo la Mtera mkoani Dodoma utakaonufaisha wananchi zaidi ya elfu saba na mia tano.

[caption id="attachment_50802" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Maji, mhe. Jumaa Aweso akizindua mradi wa maji utakaonufaisha wakazi zaidi ya 7500 katika kijiji cha Makang’wa jimbo la Mtera mkoani Dodoma Februari 8, 2020.[/caption]

“Mradi huu umetumia milioni 350 tu wakati tungetumia mkandarasi ingetumia zaidi milioni 600 na utaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi katika eneo lenu na hii ndiyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kuwa wananchi wote mnapata maji safi na salama,” alisisistza Aweso.

Akifafanua, Naibu Waziri Aweso amesema kuwa mradi huo umetekelezwa na wataalamu wa ndani kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) ikiwa ndio dhamira ya Serikali kupitia Wizara ya maji kutekeleza miradi ya maji hasa vijijini kwa kutumia wataalamu wa ndani.

  [caption id="attachment_50803" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi David Pallangyo akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji utakaonufaisha wakazi zaidi ya elfu saba na miatano katika kijiji cha Makang’wa katika jimbo la Mtera mkoani Dodoma Februari 8, 2020.[/caption]

“Serikali ya Awamu ya Tano inawajali wananchi wake hivyo pamoja na kukamilika kwa mradi huu tumeshatoa fedha kiasi cha shilingi milioni miamoja ziko kwenye akaunti tayari kwa ajili ya kuchimba visima viwili, hivyo wataalamu wetu watakuja hapa jumatatu tarehe 11 kufanya utafiti wa maeneo vitakapochimbwa visima hivyo”, alisisitiza Aweso.

Wananchi wote hakikisheni mnautunza mradi huu ili unufaishe hata vizazi vijavyo kwa kuwa fedha nyingi zimetumika katika kuutekeleza.

Naye, Mkurugenzi wa DUWASA Mhandisi David Palangyo amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa tarehe 19 Septemba2019 na umehusisha ujenzi wa vituo kumi na tatu (13) vya kuchotea maji kwenye maeneo mbalimbali katika Kijiji hicho, kununua na kufunga pampu zenye uwezo wa kuzalisha lita laki tatu na thelathini na sita kwa siku, mfumo wa nguvu za jua kwa ajili ya kuendesha pampu hizo, ununuzi na ulazaji wa mabomba ya plastiki na viungio vyake.

[caption id="attachment_50814" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Maji, mhe. Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji baada ya kuzindua mradi wa maji utakaonufaisha wakazi zaidi ya 7500 katika kijiji cha Makang’wa jimbo la Mtera mkoani Dodoma Februari 8, 2020.Fedha za utekelezaji wa mradi huo zimetolewa na Serikali kuptia Wizara ya maji na mradi kutekelezwa na DUWASA.[/caption]

Kazi nyingine ni uchimbaji na ufukiaji wa mabomba ya plastiki ya class C na viungio vyake na kulaza mabomba yenye vipenyo vya ichi 1.5 hadi inchi 6 kwa jumla ya urefu wa meta zaidi ya elfu kumi na tatu.

Akizungumzia mafaniko ya mradi huo, Mhandisi Palangyo amesema kuwa wananchi wote wa Kijii cha Makangw’a sasa wanapata maji ya bomba na pia wananchi walishirikishwa katika mradi huo kuanzia kuchagua maeneo ya kujenga vituo vya kuchotea maji na hata utekelezaji wa mradi huo

[caption id="attachment_50804" align="aligncenter" width="750"] Mbunge wa jimbo la Mtera mkoani Dodoma, Mhe. Livingstone Lusinde akishukuru Serikali na Mamalaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dodoma (DUWASA) kwa kuendelea kutatua changamaoto ya upatikanaji wa maji katika jimbo hilo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji utakaonufaisha wakazi zaidi ya elfu saba na mia tano katika kijiji cha Makang’wa jimboni humo Februari 8, 2020.[/caption]

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo hilo Livingstone Lusinde amesema kuwa wananchi wanaonufaika na mradi huo wanaowajibu wa kutunza mradi huo ili usihujumiwe.

Kwa upande wa viongozi watakaosimamia mradi huo wametakiwa kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi ya mradi huo na kutunza fedha zitakazotokana na mradi huo benki ili uwe endelevu.

Kabla ya kutekelezwa kwa mradi huo hali ya upatikanaji wa maji katika Kijiji cha Makangw’a   ilikuwa siyo wa kuridhisha, maji ya bomba yalikuwa yanapatikana katika kitongoji kimoja tu kati ya 11 na yaliwekwa na mwekezaji binafsi mwaka 2016.

      [caption id="attachment_50805" align="aligncenter" width="750"] Kwaya ya Kijiji cha Makang’wa katika jimbo la Mtera ikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji utakaonufaisha wakazi zaidi ya Elfu saba na miatano katika kijiji cha Makang’wa katika jimbo hilo Februari 8, 2020.[/caption]   [caption id="attachment_50800" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Maji mhe. Jumaa Aweso akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Makangw’a katika jimbo la Mtera mkoani Dodoma baada ya kuzindua mradi huo Februari 8, 2020.[/caption] [caption id="attachment_50812" align="aligncenter" width="750"] Wananchi wa kijiji cha Makang’wa jimbo la Mtera mkoani Dodoma wakifuatilia hotuba ya uzinduzi wa mradi wa maji katika Kijiji chao Februari 8, 2020, Mradi huo utanufaisha wakazi zaidi ya 7500 wa kijiji hicho.[/caption] [caption id="attachment_50807" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Maji mhe. Jumaa Aweso akisisitiza jambo kwa. Mbunge wa jimbo la Mtera mkoani Dodoma Mhe. Livingstone Lusinde baada ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Makang’wa jimboni humo.[/caption]   [caption id="attachment_50808" align="aligncenter" width="750"] Meneja ufundi kutoka DUWASA mhandisi Mayunga Kashilimu akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maji mhe. Jumaa Aweso kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Makang’wa jimbo la Mtera mkoani Dodoma Februari 8, 2020 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo.Fedha za utekelezaji wa mradi huo zimetolewa na Serikali kuptia Wizara ya maji na mradi kutekelezwa na DUWASA.[/caption] [caption id="attachment_50809" align="aligncenter" width="750"] Mbunge wa jimbo la Mtera mkoani Dodoma, Mhe. Livingstone Lusinde akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Maji mhe. Jumaa Aweso wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Makang’wa jimboni humo.[/caption] [caption id="attachment_50810" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi David Pallangyo akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Maji mhe. Jumaa Aweso wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Makang’wa jimbo la Mtera, Mradi huo unanufaisha wananchi zaidi ya elfu saba na miatano.[/caption]

(Picha zote na Frank Mvungi)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi