[caption id="attachment_30595" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bi. Ave Maria Semakafu akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya Insha kwa washindi wa kitaifa kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), hafla hiyo imefanyika jana mjini Dodoma .[/caption] [caption id="attachment_30587" align="aligncenter" width="812"] Afisa Elimu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. James Njowi akitoa maelezo kuhusu mashindano ya mashindano ya Insha kwa washindi wa kitaifa kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), hafla hiyo imefanyika jana mjini Dodoma .[/caption]
Wanafunzi wa shule za Sekondari hapa nchini wameibuka washindi wa Tuzo za uandishi wa Insha zinazotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC).
Akiongea mbele ya Wazazi na Walimu wa Wanafunzi waliopata ushindi wa insha hizo kwa mwaka 2017 Naibu Katibu Mkuu wa Wazara ya Elimu Dkt. Ave Maria Semakafu amesema washindi wa Tuzo hizo wametoa taswira tofauti na dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa elimu ya Tanzania si bora katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za kusini mwa Afrika.
Akifafanua Dkt. Semakafu amesema kuwa mashindano hayo ni kielelezo kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kutoa elimu bora na wanafunzi walioshinda tuzo za uandishi bora wa insha wameonyesha kwa vitendo mafanikio ya uwekezaji uliofanywa na Serikali katika sekta ya elimu.
[caption id="attachment_30588" align="aligncenter" width="797"] Mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Kagemuya ya Mkoani Kagera Bw. Arnold Matungwa akipokea zawadi kama mmoja wa washindi wa insha hiyo wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi hao jana mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_30591" align="aligncenter" width="1000"] Kaimu mratibu wa mashindano ya insha kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC ) kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bw. Salum Salum akitoa maelezo mafupi kuhusu mafanikio ya mashindano hayo jana mjini Dodoma wakati wa hafla yakuwatunuku zawadi kwa washindi wa shindano hilo.[/caption]‘’Matokeo ya Insha hizi pia yanaonesha picha tofauti na mawazo yaliyojengeka katika jamii kuwa shule binafsi ni bora kuliko shule za Serikali kwani baadhi ya wanafunzi kutoka shule za serikali wamejitokeza na kufanya vizuri katika mashindano ya uandishi wa insha.’’ Alisisitiza Dkt. Semakafu.
Mwanafunzi bora wa mashindano ya insha hizi kwa Jumuiya ya EAC ni Michael Msafiri kutoka shule ya Sekondari Kibaha ya Mkoani Pwani.
Kwa upande wake Kaimu mratibu wa mashindano ya insha kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Bw. Salum Salum amesema kuwa ushiriki wa wanafunzi katika uandishi wa insha umepanua maarifa ya wanafunzi walioshiriki katika shindano hilo.
“Maarifa ya wanafunzi yameongezeka hasa kuhusu mipango ya Jumuiya hizi na katika mchakato mzima wa mtangamano ndani ya Jumiya hizo na baina ya Jumuiya na Jumuiya” Alisisitiza Salum
Akifafanua amesema kuwa anawapongeza viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Mafunzo ya Amali Zanzibar na Baraza la Mitihani Tanzania kwa kusaidia kufanikisha mashindano hayo.
Pia alitoa wito kwa wakuu wa shule kuwasaidia wanafunzi kufuata taratibu zote za uandishi wa Insha kwa ufanisi ili kupanua wigo wa wanafunzi kushiriki katika mashindano hayo.
Hafla ya kuwatunuku tuzo washindi wa uandishi wa Insha hizo imefanyika leo mjini Dodoma ikihusisha Insha za Jumuiya ya Afrika Mashariki na zile za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).