Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waliokamatwa na Viza za Kughushi Washughulikiwe- Rais Magufuli
Nov 25, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na Jonas Kamaleki- MAELEZO, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza waliokamatwa na viza za kughushi washughulikiwe bila kujali cheo, umaarufu wala majina yao.

Agizo hilo Raisi amelitoa wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji leo jijini Dodoma.

Rais ameipongeza Uhamiaji kwa kujenga jingo zuri la kisasa ambalo liboresha utoaji wa pasipoti hasa mikoani na kuwa litpendezesha Jiji la Dodoma.

Aidha, Rais Magufuli ameonyesha kukerwa na Jeshi la Magereza kutowatumia wafungwa kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi.

“Ni aibu nyumba za askari magereza kujengwa na Jeshi la Wananchi wakati wafungwa wapo,” alisema Rais Magufuli.

Rais ameonyesha kutokubaliana na matumizi ya shilingi bilioni 8 kwa ajili ya CCTV Camera na milango ya atomatiki ya jingo hilo.

Ameongeza kuwa pamoja na mabo mengi mazuri yanayofanywa na jeshi hilo, ikiwemo pasipoti mtandao amesema hilo la bilioni 8 lifutwe na kuwataka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji kukaa na kutathmini upya na kushusha gharama za ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji.

Rais Magufuli ameipongeza Uhamiaji kwa kutunukiwa tuzo yapasipoti bora katika Ukanda wa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, kwa kukidhi viwango vya ubora wa kiusalama.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi