[caption id="attachment_36734" align="aligncenter" width="893"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mhe. Selemani Jafo akizungumza wakati akifunga semina kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashuri leo Jijini Dodoma, semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo Viongozi hao ili kuongeza tija katika maeneo yao.[/caption]
Na; Frank Mvungi
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashuri wametakiwa kuwa wabunifu kwa kutumia rasilimali zilizopo katika maeneo yao kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Akizungumza wakati akifunga semina ya siku tano kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa halmashuri iliyoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi leo Jijini Dodoma, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa Viongozi hao wanalo jukumu la kutumia rasilimali zilizopo katika maeneo yao kutatua changamoto zinazowakabili wananchi .
‘Kuna umuhimu mkubwa kwenu kama viongozi kushughulikia kero za wananchi kwa kushirikiana na wale walio chini yenu wakiwemo watendaji katika ngazi ya Kata na Vijiji na sikusubiri mpaka viongozi wa Kitaifa wafike katika maeneo yenu ndio watoe majibu ya changamoto za wananchi”; Alisisitiza Jafo
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge akizungumza wakati wa hafla ya kufunga semina kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri leo Jijini Dodoma, semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo Viongozi hao ili kuongeza tija katika maeneo yao.
Akifafanua Mhe. Jafo amesema kuwa mabadiliko katika Mamlaka za Serikali za mitaa yataletwa na watendaji hao ambapo aliwataka kufanya kazi kwa kujituma na bila kuchoka kwa kuwa wananchi wana matarajio makubwa kutoka kwa watendaji wote katika Wilaya na Halmashuri zote nchini.
“ Tufanye kazi itakaoweka alama katika maeneo yetu hasa katika kusimamia maadili, manunuzi, sheria kanuni, taratibu na mipango yote inayopangwa na Serikali ikilenga kuwaletea wananchi maendeleo kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.”Alisisitiza Jafo
Aliongeza kuwa tayari Serikali imetoa bilioni 33 kwa ajili ya ujenzi wa Hosipitali za Wilaya 67 ambapo zitasaidia kuboresha huduma za afya kwa wananchi, sambamba na ujenzi wa vituo vya afya 348 ambapo vituo 210 vimeshakamilika.
Katika kuimarisha huduma kwa wananchi TAMISEMI imeendelea kufanya mapinduzi makubwa katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, Afya, Shule ambapo Waziri Jafo amesisitiza umuhimu kwa viongozi hao kuhakikisha kuwa miradi yote inayoteklezwa katika maeneo yao inaendana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa na si vinginevyo.
[caption id="attachment_36736" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Idara ya Elimu kwa Viongozi kutoka Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo akizungumza wakati wa kufunga semina kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashuri leo Jijini Dodoma, semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo Viongozi hao ili kuongeza tija katika maeneo yao.[/caption]Waziri Jafo amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa wanasimamia kikamilifu fedha za maendeleo zinazotolewa na Serikali ili kuepusha matumizi yasiyo sahihi ya rasiliamli hizo ambazo zinatolewa na Serikali kwa lengo la kuleta mageuzi ya kweli katika maisha ya wananchi.
Jambo jingine Muhimu alilosisitiza ni kusimamia ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao ili kuchochea maendeleo hasa kuboresha maisha ya wananchi.
Aidha, Mhe. Jafo aliagiza kuwa watendaji ambao wanashindwa kutekeleza majukumu yao katika Halmashuri waondolewe mara moja ili kuwapa nafasi wale wenye uwezo kushika nafasi hizo.
Pia aliwataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuzingatia mipaka ya kazi na kuheshimu mamlaka zote ili kuongeza tija katika maeneo yao.
Katika kukabiliana na changamoto zilizopo kama madawa ya kulevya, Waziri Jafo amesema kuwa Wakuu wa Wilaya wahakikishe kuwa wanasimamia mapambano hayo katika maeneo yao kwa nguvu zao zote.“ Wakuu wa Wilaya kasimamieni ulinzi na usalama katika maeneo yenu, hizi ni agenda muhimu katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwa haya ndiyo yanayochagiza kufanikiwa kwa dhana ya ujenzi wa uchumi jumuishi”. Alisisitiza Mhe. Jafo
Semina kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri imefanyika Jijini Dodoma kwa siku 5 ikilenga kuwajengea uwezo katika kutekelza majukumu yao mara baada ya kuteuliwa hivi karibuni.
[caption id="attachment_36737" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Msuya akizungumza wakati wa hafla ya kufunga semina kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri leo Jijini Dodoma, semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo Viongozi hao ili kuongeza tija katika maeneo yao.[/caption] [caption id="attachment_36740" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya Wakuu wa Wilaya wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo wakati akifunga semina kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashuri leo Jijini Dodoma, semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo Viongozi hao ili kuongeza tija katika maeneo yao.[/caption] [caption id="attachment_36739" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya watoa mada wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo wakati akifunga semina kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashuri leo Jijini Dodoma, semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo Viongozi hao ili kuongeza tija katika maeneo yao.[/caption] [caption id="attachment_36735" align="aligncenter" width="885"] . Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe akizungumza wakati wa hafla ya kufunga semina kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi leo Jijini Dodoma, semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo Viongozi hao ili kuongeza tija katika maeneo yao na Imeandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi.[/caption](Picha zote na Frank Mvungi)