Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wakurugenzi Njombe Wafunguka Mafanikio Awamu ya Sita
Dec 21, 2023
Wakurugenzi Njombe Wafunguka Mafanikio Awamu ya Sita
Baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri mbalimbali wa mkoani Njombe wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Wakurugenzi wa Halmashauri na Waandishi wa Habari leo tarehe 21 Desemba 2023.
Na Mwandishi Wetu - MAELEZO

Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri mbalimbali mkoani Njombe wameeleza mafanikio yaliyopatikana katika Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Wateule hao wenye mamlaka ya kusimamia miradi ya maendeleo wameanika mafanikio hayo leo mjini Njombe wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari.

"Tumepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi ambayo imeshajengwa na tumefanya marekebisho kwenye ofisi za watendaji wa kata," ameeleza Ndg. Sunday Deogratius, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ludewa.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Njombe Mji, Ndg. Thadei Luoga amesema watumishi wa halmashauri hiyo wameboreshewa mazingira ya kufanyia kazi kwa kupewa vyombo vya usafiri zikiwamo pikipiki.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Makete, Ndg. William Mafyukwe amesema wanajipanga kuzalisha tani laki mbili za ngano kwa mwaka ifikapo 2027.

Tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 Rais Samia amekuwa akiwahimiza wakurugenzi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali na kusogeza karibu huduma za jamii huku akiteua viongozi wapya ili wamsaidie kutekeleza kazi kwa ufanisi zaidi

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi