[caption id="attachment_7183" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kwanza Kulia) akisalimiana na Wakina Mama wa Kijiji cha Msangambuye wakati wa Ziara yake Wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe.
Nteghenjwa Hosseah-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuandaa mazingira rafiki kwa watumishi wapya wanaopangiwa katika Halmashauri zao.
Simbachawene ameyasema hayo ikiwa ni wiki moja tangu kutangaza ajira mpya za Walimu wa Masomo ya Hisabati na Sayansi wapatao 3,081 wa ngazi ya Shahada na Stashahada ambao wamepangiwa kwenye Halmashauri mbalimbali Nchini.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msangambuya wakati wa Ziara yake ya Kikazi Wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe Mhe. Simbachawene amesema watumishi wengi wapya wanakatishwa tamaa na mazingira mabovu wanayoyakuta katika Halmashauri zao na hali hiyo huwatia hofu ya kuendelea kukaa katika maeneo hayo.
“Unakuta mtumishi anafika Halmashauri malipo yake hayajaandaliwa zaidi ya mwezi mzima, kisha anapangiwa kwenye kata mbayo hata hajawahi kuifahamu hapo awali na hapewi hata maelekezo ya ziada ya namna ya kufika katika Kituo chake na unakuta wenyeji wake katika Kata na Shule hawana taarifa za ujio wa mtumishi huyon hivyo mtumishi anahangaika mpaka anakosa ari ya kufanya kazi katika kituo chake kipya,” alisema Simbachawene.
“Ninahitaji Kila Halmashauri kuandaa malipo stahiki kwa ajili ya walimu wanaoendelea kuripoti hivi sasa katika maeneo mbalimbali, usafiri wa kuwapeleka katika vituo vyao vya Kazi, mapokezi stahiki kwa uongozi wa kata, shule pamoja na kuhakikisha walimu hao wanapata makazi bora ya kuishi katika maeneo yao mapya ya kazi”.
[caption id="attachment_7191" align="aligncenter" width="750"] Mama Theresia Costantine Komba (kushoto) akimshkuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene kuwatembelea katika Kijiji cha Chinoje.[/caption]Ameendelea kwa kusema kuwa, hataielewa Halmashauri ambayo itashindwa kuzingatia maagizo hayo kwa namna yoyote ile na ataendelea kufuatilia mazingira ya mapokezi ya watumishi hao.
Aidha amesema, hataki kuona mtumishi yeyote anashindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi kwa sababu ya mazingira magumu anayokutana nayo wakati wa kuripoti kazini.
Kwa upande wake, kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri hiyo Bi. Eliachi Macha alisema, Halmashauri hiyo imeandaa mazingira mazuri kwa ajili ya mapokezi ya walimu wapya na wanatekeleza maagizo yote yaliyoliyotolewa ili watumishi wote waweze kufanya kazi za ujenzi wa Taifa na kuleta matokeo chanya kwa Taifa.
Nae, Diwani wa Kata ya Mtera Mhe. Amon Kodi ambaye alishiriki katika ziara hiyo amempongeza Waziri Simbachawene kwa kazi kubwa anayoendelea kufanya katika Kata yao, Jimbo la Kibakwe na Taifa kwa Ujumla.
Vile vile, amemshukuru kwa kufanikisha utekelezaji wa Miradi ya ujenzi wa bweni la Mtera Sekondari, ukarabati wa zahanati ya kisima pamoja na ukarabati wa matundu ya vyoo vya Shule ya Msingi Msangambuya.
Mhe. Simbachawene yupo katika ziara ya Kikazi Wilayani Mpwapwa, Jimbo la Kibakwe na ametembelea Kijiji cha Msangambuya, Chamsisili pamoja na Chinoje.