[caption id="attachment_39093" align="aligncenter" width="900"] Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Bw. Wilson Malosha akisisitiza jambo wakati akifungua warsha ya siku moja kwa wadau wa sekta ndogo ya uzalishaji na usindikaji wa alizeti hapa nchini iliyoandaliwa na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) leo Jijini Dodoma na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka katika taasisi na mikoa mbalimbali. Warsha hiyo ililenga kujadili mafanikio yaliyopatikana baada ya Serikali kuongeza ushuru wa forodha wa asilimia 25 kwenye mafuta ghafi ya kula yanayoagizwa kutoka nje ya nchi.[/caption]
Na; Mwandishi Wetu
Wakulima na Wasindikaji wa mafuta ya alizeti wametakiwa kutumia taarifa za tafiti mbalimbali kusaidia katika kukuza sekta hiyo ambayo ina mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Akizungumza wakati akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) Jijini Dodoma kwa wasindikaji na wawakilishi wa wakulima wa zao hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Bw. Wilson Malosha amesema kuwa ni vyema wazalishaji hao na wakulima wakatumia tafiti mbalimbali zilizofanyika kuongeza tija .
[caption id="attachment_39094" align="aligncenter" width="897"]Warsha hiyo ililenga kujadili mafanikio yaliyopatikana baada ya Serikali kuongeza ushuru wa forodha wa asilimia 25 kwenye mafuta ghafi ya kula yanayoagizwa kutoka nje ya nchi.
‘’ Kila mmoja katika eneo lake ana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa anachangia katika kuiwezesha nchi yetu kupunguza au kuondoa utegemezi wa mafuta ya kula kutoka nchi za nje kwa kuongeza uzalishaji wenye tija kwa kutumia alizeti tunayozalisha”.Alisisitiza Malosha
Akifafanua amesema kuwa mikakati ya pamoja inahitajika kati ya wazalishaji na Serikali ili kuwezesha azma yakukuza uzalishaji wa mafuta na alizeti kukua kwa kasi inayoendana na mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi ili kuchangia katika kukuza uchumi.
[caption id="attachment_39096" align="aligncenter" width="900"]Aliongeza kuwa Taifa letu limejaliwa ardhi yenye rutuba kwa ajili ya uzalishaji wa zao hilo na kutaja baadhi ya mikoa hiyo kuwa ni Morogoro na Singida.
Kuongeza uzalishaji katika sekta hiyo kutachochea maendeleo ya viwanda na kupunguza fedha za kigeni zinazotumika katika kuagiza mafuta nje ya nchi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha wasindikaji wa alizeti Bw. Ringo Iringo amesema kuwa warsha hiyo itasaidia kuja na mikakati ya pamoja na kila mdau ataona eneo analopaswa kuchukua hatua katika kuhakikisha kuwa sekta hiyo inakua na kuchangia katika kukuza uchumi.
[caption id="attachment_39099" align="aligncenter" width="808"]Aliongeza kuwa vikosi kazi vilivyoundwa kupitia Baraza la Biashara la Taifa vitatoa mchango mkubwa katika kutoa mapendekezo ya namna bora ya kutatua changamoto zilizopo ili kukuza sekta hiyo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. amesema kuwa Semina hiyo imewashirikisha viongozi wa vyama vya wazalishaji na wasindikaji wa alizeti wa mikoa takribani 19.
Warsha hiyo imeshirikisha Ofisi ya Waziri Mkuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wawakilishi wa wakulima wa alizeti na wasindikaji wa alizeti kutoka katika mikoa takribani 19 ya hapa nchini.