Wakazi Mkoani Mwanza Wapatiwa Elimu ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii
Nov 22, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Sehemu ya washiriki na wakazi wa Mwanza wakiwa kwenye viwanja vya Rock City Mall wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Hifadhi ya Jamii, Bw. Omary Mziya (hayupo pichani) wakati wa zoezi la uelimishaji umma katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, Jijini Mwanza.
Afisa Uhusiano kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Abdul Njaidi akitoa elimu kwa wakazi wa Mwanza kuhusu huduma zinazotolewa na mfuko huo wakati wa zoezi la uelimishaji umma katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika viwanja vya Rock City Mall, Mwanza.