Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wakati wa Kunufaika na Sanaa ni Sasa- Dkt. Mapana
Dec 05, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa BASATA, Dkt. Kedmon Mapana akizungumza wakati akifungua kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa Tamasha la Utoaji Tuzo la Uni Awards msimu wa nne 2022 leo Desemba 4, 2022 katika ukumbi wa JNICC Dar es salaam.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa BASATA, Dkt. Kedmon Mapana amesema Serikali ya Awamu ya Sita imetoa nafasi na fursa nyingi kwa sekta za utamaduni na sanaa ambazo zimeweza kutoa ajira kwa vijana wengi kwa wakati mmoja.

Dkt. Mapana ameyasema hayo wakati akifungua kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa Tamasha la Utoaji Tuzo la Uni Awards msimu wa nne 2022 leo Desemba 4, 2022 katika ukumbi wa JNICC Dar es salaam.

Amesema kuwa tasnia imewekewa mazingira mazuri kuanzia kwa Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wa Wizara, hivyo ni wakati sahihi kwa kufanya uwekezaji kwenye sekta ya sanaa ili kukuza uchumi na Serikali imeahidi kuwa sambamba ili Uni Awards iwe ya kimataifa.

Ameongeza kuwa sekta hii imethibitika kuongeza pato la nchi kwa asilimia 19, hivyo haipaswi kubezwa isipokuwa kutiliwa mkazo katika ubunifu kwa kuwa inaaminika Tanzania itakuwa maradufu kisanaa baada ya Nigeria kwa sasa.

Juu ya hapo amewatia moyo wanachuo kuwa sanaa ya nchi imezidi kushika kasi katika majukwaa ya kimataifa akitolea mfano Tuzo ya Afrimma aliyokabidhiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakati huohuo, mratibu wa tuzo hizo, Bi. Shine Basil ameishukuru Serikali kwa namna inavyojitoa kuhakikisha tamasha linafanyika na kwa kuwa linakutanisha vijana kutoka vyuo mbalimbali hivyo linawajengea msingi imara wa kutambua ajira katika sekta ya Sanaa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi