Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wajumbe wa TEITI Watakiwa Kutekeleza Majukumu yao kwa Weledi na Uzalendo
Oct 25, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37409" align="aligncenter" width="894"] Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb)akisisitiza kuhusu wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo.[/caption]

Frank   Mvungi- MAELEZO

Kamati ya Uhamasishaji  Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali na Madini, Mafuta na Gesi asilia nchini (TEITI) imetakiwa kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uzalendo kwa maslahi ya Taifa.

Akizungumza  wakati  akizindua Kamati hiyo Waziri wa Madini Mhe. Angellah  Kairuki (Mb) amesema kuwa msingi wa falsafa ya uwazi na uwajibikaji kwenye sekta ya uziduaji umejikita kwenye Ibara ya 8 (1) (C) na Ibara ya 27 (1) and (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 .

“ Ibara hizi zinazungumzia Serikali kuwajibikaji kwa wananchi wake na kwamba rasilimali zote za nchi zitatunzwa na wananchi wote kwa manufaa ya wote, Aidha Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia Tanzania ya mwaka 2015 nayo imeweka msingi imara wa kuhakikisha kunakuwa na uwazi na uwajibikaji kwenye sekta ya uziduaji”; Alisisitiza Mhe. Kairuki

[caption id="attachment_37410" align="aligncenter" width="868"] Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb)akizungumzia umuhimu wa sekta ya gesi katika kukuza uchumi kwa wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo.[/caption]

 “Mwenyekiti na wajumbe mtambue kuwa mmepewa mamlaka makubwa na mmeaminiwa kulinda maslahi ya nchi  kwa kusimamia Sheria ya uwazi na uwajibikaji katika rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia Tanzania ya mwaka 2015 na vigezo vya Kimataifa vya uwazi ( Extractive Industries Transparency Initiative (EITI) Requirements)”; Alisisitiza Mhe. Kairuki

Alibainisha kuwa kila ,mtanzania kwa sasa ni shahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ilivyo na dhamira ya dhati kuona kwamba sekta ya uziduaji inawanufaisha watanzania wote kwa kuhakikisha kuwa Serikali inapata mapato yake stahiki na wananchi wanashiriki kikamilifu kiatika usimamizi wa rasilimali za nchi yao.

[caption id="attachment_37411" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani wakimkabidhi vitendea kazi mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini Bw. Ludovick Utouh leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo.[/caption]

Akizungumzia majukumu ya Kamati hiyo Mhe. Kairuki amesema kuwa moja ya majukumu ya Kamati hiyo ni kuandaa mfumo wa  uwekaji uwazi na uwepo wa uwajibikaji kwa mali[o yaliyofanywa na Kampuni za uziduaji kwa Serikali,kuhamasisha ufahamu juu ya mchango wa sekta ya uziduaji na maendeleo yake kiuchumi na kijamii pamoja na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika sekta ya uziduaji.

Majukumu mengine ni pamoja na kuzitaka kampuni za uziduaji kuwasilisha kwenye Kamati gharama za uwekezaji, takwimu  za uzalishaji na mauzo ya Nje katika mwaka husika wa fedha.

[caption id="attachment_37412" align="aligncenter" width="900"] . Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini Bw. Ludovick Utouh akizungumzia wajibu wa Kamati hiyo na jinsi ilivyojipanga kutekeleza majukumu yake leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo.[/caption]

Kwa upande wake Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.  Medard  Kalemani amesema kuwa rasilimali za mafuta na gesi zinapaswa kutoa mchango unaotakiwa katika kukuza uchumi wa Taifa.

Aliongeza kuwa mapato ya sekta ya gesi yameongezeka kufikia bilioni 29.4 kwa mwaka kutoka bilioni 8 zilizokuwa zikikusanywa awali.

Kuongezeka kwa mapato hayo ni matokeo yakufanyika kwa maboresho katika sheria na kutungwa kwa sheria ya ulinzi wa rasilimali za Taifa mara baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani.

Naye Mwenyekiti wa  TEITI Bw. Ludovick utouh amesema kuwa Kamati hiyo itafanaya kazi kwa weledi kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

Alishukuru kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kuahidi kushirikiana na Wizara ya Madini na ile ya Nishati kutatua changamoto zilizopo katika sekta hizo ili ziweze kutoa mchango wake kikamilifu katika ujenzi wa uchumi na ustawi wa Taifa.

TEITI ina umuhimu mkubwa katika kuliwezesha Taifa kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka  2025 kupitia ujenzi wa uchumi wa Viwanda , Kamati hii ilianza mwaka 2009.

[caption id="attachment_37413" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb)akisisitiza kuhusu umuhimu wa wananchi kushirikiana na Serikali kuwafichua wale wote wanashiriki katika vitendo vya kuhujumu sekta ya madini, gesi na mafuta ili Serikali ichukue hatua stahiki.[/caption] [caption id="attachment_37414" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya wajumbe na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37415" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini leo Jijini Dodoma mara baada ya kuzinduliwa kwa Kamati hiyo.[/caption] [caption id="attachment_37416" align="alignnone" width="900"] Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Kamati ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini leo Jijini Dodoma.
                                                                                                                    (Picha zote na Frank Mvungi)[/caption]    

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi