Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wajasiriamali Watakiwa Kuthibitisha Ubora wa Bidhaa zao
Dec 06, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi Wetu

WADAU wa mikutano ya mashauriano kati ya Serikali, wafanyabiashara na wawekezaji wamepatiwa elimu kuhusiana na majukumu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), fursa ya wajasiriamali kupatiwa bure alama ya ubora pamoja na kuzipatia ufumbuzi wa changamoto zinawakabili. Mikutano hiyo ya mashauriano kwa mikoa ya Kanda ya Pwani iliyoanza Desemba 4, mwaka na kuhudhuriwa na mawaziri na manaibu waziri takribani 13 ni mwendelezo wa mikutano iliyotangulia inayolenga kuzipatia ufumbuzi changamoto za zinaziwakabili wafanyabiasha na wawekezaji. Mikoa hiyo ya Kanda ya Mashariki ni Morogoro, Pwani wenyewe na leo mikutano hiyo ilihitimishwa jijini Dar es Salaam. Katika mikutano Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Yusuf Ngenya, aliwapatiwa elimu wadau hao kuhusu fursa wanazopata wafanyabiashara na wazalishaji ambao bidhaa zao zimekidhi viwango vya ubora, kuhamasisha wajasiriamali kuthibitisha ubora wa bidhaa zao bure pamoja na kuzipatia majibu changamoto wanazokumbana wadau wake mbalimbali. Dkt. Ngenya alitaja fursa zinazotolewa na shirika hilo kwa wajasiriamali ambazo ni pamoja kuthibitisha ubora wa bidhaa wanazozalisha bila malipo kwa miaka mitatu lengo likiwa ni kuwawezesha kupanua soko la bidhaa zao na kuwaondolea vikwazo vya kibiashara. Alisema Serikali imeanzisha utaratibu huo ili kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa zenye ubora na kupanua wigo wa masoko hayo. Alitoa wito kwa wajasiriamali na wananchi kwa ujumla kuchangamkia fursa hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inasisitiza ujenzi wa uchumi wa viwanda. “TBS kama taasisi wezeshi inatoa huduma ya kuthibitisha ubora wa bidhaa bure kwa wajasiriamali wadogo na wakati, lengo likiwa ni kuendeleza viwanda vya Tanzania, hivyo ni vyema wakathibitisha ubora wa bidhaa zao ili wasipate vikwazo vyovyote katika kupata soko ndani na nje ya nchi,” alisema Dkt. Ngenya. Alisema kuwa endapo wajasiriamali hao watathibitisha bidhaa zao itawasaidia kuzalisha bidhaa endelevu ambazo zitakuwa na soko kila mahali ikiwemo masoko ya kikanda. Dkt. Ngenya, alifafanua kuwa lengo la TBS ni kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zenye tija kwa taifa, bila kuathiri taratibu na sheria za nchi. Kutokana na umuhimu huo, alisema ndiyo maana shirika hilo limeshiriki mikutano hiyo kama taasisi wezeshi. Alisema Shirika litaendelea kutoa elimu ya viwango kwa Watanzania wote lengo kuu likiwa ni kuwa na uwelewa wa pamoja wa masuala ya viwango na ubora wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi na zile zinaingizwa kutoka nje nchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi