[caption id="attachment_41569" align="aligncenter" width="1008"] Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mh. Kissa Gwakisa akifungua semina ya wajasiriamali juu ya utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS.[/caption]
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha eneo lililotengwa kwa ajili ya wajasiriamali linaanza kufanyiwa maandalizi ya awali ili kuondoa changamoto ya eneo la kuzalisha kwa mjasiriamali mdogo.
Alitoa maagizo hayo wakati akifungua mafunzo ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa wajasiriamali wadogo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, ambapo wajasiriamali 104 walihudhuria.
Gwakisa alisema eneo la uzalishaji ni kilio cha wazalishaji wadogo wengi na hivyo hatua hiyo itawasaidia wajasiriamali hao kupata alama ya ubora wa bidhaa wanazozalisha.
Kwa upande wake, Afisa masoko mwandamizi wa TBS, Bi. Gladness Kaseka, alitoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya kwa kuwajali wajasiriamali hao kwani itawasaidia kupata leseni ya kutumia alama ya ubora na vilevile huduma hiyo kwa mjasiriamali mdogo ni bure.
[caption id="attachment_41568" align="aligncenter" width="1008"] Afisa Masoko mwandamizi Bi. Gladness Kaseka (TBS) akitoa elimu ya Viwango kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyerere wilayani Korogwe.[/caption]Kaseka aliwakumbusha kuomba mafunzo maalum TBS, ambapo TBS hufanya kushirikiana na SIDO na TFDA bila gharama yoyote.
Wajasiriamali waliopata elimu hiyo wamefurahishwa na Shirika hilo kuwafikia na kuwaongezea uelewa wa viwango na kuwajulisha juu ya fursa ya bure kwao kupata leseni ya TBS itakayowasaidia kuuza bidhaa zao popote na ushindani halali sokoni.
Sambamba na mafunzo hayo Shirika pia lilitoa elimu ya viwango kwa wananchi katika maeneo ya stendi ya zamani ya manundu, stendi mpya, soko la manundu na sabasaba, pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Nyerere yenye jumla ya wanafunzi na walimu 746.
[caption id="attachment_41570" align="aligncenter" width="1008"] Wajasiriamali wilayani Korogwe wakipata elimu juu ya utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS .[/caption]