[caption id="attachment_3967" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kati ya TFDA, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), SIDO, na TANTRADE kilichofanyika hivi karibuni kikilenga kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kutatua changamoto zinazowakabili wajasiriamali hapa nchini. (Picha na: TFDA)[/caption]
Na. Frank Mvungi.
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeandaa mkakati wa kuwasaidia wajasiriamali nchini kukabiriana na changamoto zinazokwamisha maendeleo yao ili waweze kuchangia juhudi za Serikali katika kujenga uchumi wa viwanda.
Mkurugenzi wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo ameeleza hivi karibuni kuwa miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali kwa kushirikiana na taasisi zingine ambazo kwa njia moja au nyingine zinagusa shughuli za wajasiliamali nchini.
Alizitaja taasisi hizo kuwa ni Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) na GS1, ambazo kwa pamoja zitakuwa zikitoa mafunzo ya namna ya kuboresha bidhaa za wajasiriamali ili ziendande na mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
“Changamoto zinazowakabili wajasiriamali ni mtambuka na zinahitaji mikakati ya pamoja ya sekta na wadau katika kukabiliana nazo”. Alisisitiza Sillo wakati wa kikao cha pamoja na taasisi hizo.
Ametaja mkakati mwingine ni kuundwa kwa Kamati ya wataalam nane ambayo itaratibu namna ya kutekeleza mikakati ya kuondoa changamoto zinazowakabili wajasiriamali kote nchini. Kamati hiyo itajumuisha wajumbe wawili kutoka kila taasisi.
[caption id="attachment_3968" align="aligncenter" width="751"] Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo wa kwanza kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mhandisi Agnes Kiwelu (katikati) na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Prof. Sylvester Mpanduji na mwisho kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Bw. Edwin Rutagaruka.[/caption]Pia Bw. Sillo amezishauri TanTrade na SIDO kufuatilia katika halmashauri zote nchini upatikanaji wa maeneo ya uzalishaji yatakayotumiwa na wajasiriamali hao ili kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa vitendo.
Kwa upande wa bidhaa hatarishi (high risk food products), Mkurugenzi wa TFDA amesisiza bidhaa hizo zisizalishwe bila kuwa na vibali kutoka TFDA ili kulinda afya ya mlaji na mamlaka hiyo kufanya marejeo ya kanuni ya ada na tozo ni mkakati wa kuweka unafuu kwa wajasiriamali.
Kuanzia mwaka 2013/14 hadi 2016/17, TFDA imetoa mafunzo kwa wajasiliamali katika mikoa 16 ambayo ni Dar es Slaam, Pwani, Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma na Rukwa.
Mikoa mingine ni Manyara, Lindi, Mtwara, Tanga, Singida, Iringa, Kigoma, Kilimanjaro na Morogoro.
Aidha jumla ya wajasiriamali 1,287 wameisha pewa mafunzo mapaka kufikia mwezi June, 2017 ambapo kwa sasa mafunzo hayo yatafanyika kwa kushirikisha taasisi zote zenye jukumu la kuwahudumia wajasiriamali hapa nchini.