Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Wafamasia nchini waaswa kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kutoa huduma bora kwa wananchi hasa wanyonge itimie kwa wakati.
Akizungumza katika mahojiano maalum leo Jijini Dodoma kuhusu maadhimisho ya siku ya wafamasia Duniani, Msajili wa Baraza la Famasi Tanzania Bi Elizabeth Shekalaghe amesema kuwa maadhimisho ya siku ya wafamasia yanalenga kufanya tathmini ya utendaji wao ili kuona namna bora ya kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Msajili wa Baraza Famasi Tanzania Bi Elizabeth Shekalaghe (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bw. Juma Mnwele leo Jijini Dodoma wakati alipotembelea Banda la Baraza hilo lililopo katika Viwanja vya Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
“Siku hii ni muhimu kwa Wafamasia wote kwani inatuleta pamoja si tu kusherehekea bali kuangalia na kufanya tathmini ya kina kuhusu utendaji wetu wa kila siku katika kuwahudumia wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na hatimaye tuendelee kuboresha utendaji wetu” .Alisisitiza Bi Shekalaghe
Akifafanua amesema kuwa, jukumu la kutoa huduma bora kwa wananchi ni nyenzo muhimu katika kuchochea ukuaji wa kada hiyo na ustawi wa jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Kahama Bw. Anderson Msumba akisisitiza jambo kwa Msajili wa Baraza Famasi Tanzania Bi Elizabeth Shekalaghe leo Jijini Dodoma ikiwa ni siku ya wafamasia Duniani ambapo Baraza hilo linashiriki kutoa elimu kwa wajumbe wa mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) leo Jijini Dodoma.
Pia alitoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kupata huduma katika maduka yaliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zinazosimamia kada hiyo.
Baraza la Famasi ni taasisi ya kitaaluma chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, lililoundwa chini ya kifungu Na. 2 cha Sheria ya Famasi Cap 311 baada ya Sheria ya Famasi ya mwaka 2002 kufutwa. Baraza limepewa jukumu la kusimamia taaluma ya famasi ikiwemo usajili wa maduka ya dawa kazi ambayo imeanza kutekelezwa rasmi mwaka 2012. Katika kutekeleza Sheria ya Famasi, Baraza linashirikiana na watendaji wa Halmashauri na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
[caption id="attachment_35673" align="aligncenter" width="834"] Msajili wa Baraza Famasi Tanzania Bi Elizabeth Shekalaghe akiwa kwenye picha ya pamoja na wafamasia wa Baraza hilo wanaoshiriki kutoa elimu kuhusu majukumu ya Baraza hilo katika mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) leo Jijini Dodoma.[/caption]Sehemu ya majukumu ya Baraza hili ni Kusajili wanataaluma wote (Wafamasia) , Kusajili majengo ya kutolea huduma za dawa, Kuweka na kusimamia viwango vya utendaji wa taaluma ya famasi , Kupitia mitaala na kuweka viwango vya elimu kwa wanataaluma wa famasi na kuhakikisha vina ubora unaohitajika, Kuhamasisha na kusimamia maadili ya taaluma ya famasi .
[caption id="attachment_35675" align="aligncenter" width="900"] Mfamasia wa Baraza la Famasi Tanzania Bi Suma Jairo akisisitiza jambo kwa mmoja wananchi waliotembelea Banda la Baraza hilo lililopo katika Viwanja vya Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.[/caption]Majukumu mengine ni Kujibu na kushughulikia masuala yote yanayohusu taaluma ya famasi , Kulinda na kuhamasisha huduma za taaluma ya famasi zitolewe kulingana na viwango na maadili, Kuweka na kutunza taarifa za wanataaluma wote waliosajiliwa, Kuimarisha uhusiano na ushirikiano na taasisi
Msajili wa Baraza Famasi Tanzania Bi Elizabeth Shekalaghe akisisitiz jambo kwa Maofisa wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA) leo Jijini Dodoma ikiwa ni siku ya wafamasia Duniani , Baraza hilo linashiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) unaoendelea Jijini Dodoma.