[caption id="attachment_8845" align="aligncenter" width="750"] Mtafiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Milemine East Refining Bw. Salvatory Rwebangila akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea jitihada za Rais John Magufuli katika kutetea rasilimali za taifa na kuokoa upotevu wa mapato, kushoto ni Afisa uhusiano wa Taasisi hiyo Bi. Oliver Rwebangila na kushoto ni Afisa Mipango wa taasisi hiyo Bw. Respikius Antony. (Picha na: Eliphace Marwa)[/caption]
Na. Thobias Robert
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezidi kupongezwa na wadau mbalimbali wa maendeleo juu ya hatua anazozichukua katika kuliletea Taifa mabadiliko na maendeleo katika sekta mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Milemine East Refining, Salvatory Rwebangila amesema Mh.Rais amefanya mambo mengi ya kupongezwa tangu aingie madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
“Siku chache alizokaa madarakani ameweza kununua ndege kwa ajili ya Nchi hii ambayo ilibakia ndoto baada ya kupoteza ndege zilizokuwepo awali, kwani alipoingia madarakani shirika la ndege lilikuwa na ndege moja tu, unaweza kujiuliza kwa miaka yote hiyo tulikuwa wapi? Kwa kipindi hiki kifupi fedha zimepatikana wapi?” Alihoji Rwebangila.
Aidha, Rwebangila alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeondoa wafanyakazi hewa zaidi ya elfu 19 pamoja na wafanyakazi wenye vyeti feki, waliokuwa wananeemeka na rasilimali za nchi kwa njia zisizo halali. Aliongeza kuwa rais ameokoa vijana wengi katika vita yake dhidi ya madawa ya kulevya yaliyokuwa yanaangamiza nguvu kazi ya Taifa.
[caption id="attachment_8846" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mtafiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Milemine East Refining Bw. Salvatory Rwebangila (Katikati) wakati akielezea jitihada za Rais John Magufuli katika kutetea rasilimali za taifa na kuokoa upotevu wa mapato mapema hii leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]“Rasilimali za madini zilikuwa zikisombwa kwa makontena na kuiacha nchi na zawadi ya mashimo. Msimamo thabiti wa Dkt. Magufuli umemfanya kiongozi mkuu wa kampnui ya Barrick kupanda ndege binafsi kuja kuangalia jinsi ya kurudisha fedha zilizotokana na udanganyifu uliofanywa na Kampuni ya ACACIA kwenye madini ya Tanzania,” alieleza Rwebangila.
Mbali na mambo mengi ambayo Mh.rais amefanya, Rwebangila amempongeza kwa kuanzisha ujenzi wa reli ya kisasa (Standard gauge) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, kuboresha huduma za kijamii pamoja na uamuzi wake kuhamishia Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma.
“Ninampongeza Mhe. Rais kwani utume wake umeinua watu ambapo sikudhani kwamba bado tuna watu wa Mungu wenye uaminifu mkubwa wa kuyaona masuala ya hujuma mbalimbali za rasilimali za nchi na watanzania wengi wamepata mbegu mpya ya kulithamini taifa lao,” alieleza Rwebangila.
Kampuni ya Milemine East Refining yenye makao yake Jijini hapa hujishughulisha na utafiti juu ya malighafi za viwandani, madawa ya mimea, ubunifu wa teknolojia na maji kuanzia miaka ya 1980.