Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wadau Sekta ya Mafuta na Gesi Washauriwa Kujiunga na ATOGS
Aug 02, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_8189" align="aligncenter" width="750"] Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) Abdulsamad Abdulrahim akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu fursa mbalimbali zilizopo katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania, kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Dkt. Godfrey Simbeye na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Juliana Pallangyo.[/caption]

Na Jacquiline Mrisho .

Wadau wa Sekta ya Mafuta na Gesi wameshauriwa kujiunga na Jumuiya ya Watoa Huduma wa Sekta ya Mafuta na Gesi (ATOGS) ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali kwa urahisi.

Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Dkt. Julia Pallangyo aliopokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu umuhimu wa Jumuiya hiyo.

Mhandisi Dkt. Julia amesema kuwa Sera ya Taifa ya Nishati ya mwaka 2015 inahamasisha ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Mafuta na Gesi asilia hivyo uanzishwaji wa ATOGS umekua msaada mkubwa katika utekelezaji wa Sera hiyo pamoja na kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika Sekta hiyo.

[caption id="attachment_8190" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo (kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) fursa mbalimbali zilizopo katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Tanzania hadi Uganda, katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo (kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) fursa mbalimbali zilizopo katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania, katikati ni Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi watoa huduma ya mafuta na gesi nchini Abdulsamad Abdulrahim na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Dkt. Godfrey Simbeye.[/caption]

“Natoa wito kwa watoa huduma kujiunga na ATAGOS kwa kuwa kufanya hivyo kutawawezesha kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo ambao utatoa fursa mbalimbali” Dkt. Julia alisema.

Alizitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na ujenzi, uhandisi, manunuzi na uwezeshaji pamoja na huduma za kifedha na kibenki, huduma za bima, huduma kisheria, ulinzi pamoja na chakula.

Kwa upande mwingine, Naibu Katibu Mkuu amewakaribisha wananchi wa Tanga na wa mikoa ya pembezoni kufika katika eneo la Chongoleani Jumamosi tarehe 5 Agosti mwaka huu kushuhudia uwekwaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania.

[caption id="attachment_8191" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Dkt. Godfrey Simbeye akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu fursa mbalimbali zilizopo katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi linalojengwa kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania, kulia ni Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) Abdulsamad Abdulrahim na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo.[/caption]

Akimuwakilisha Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Mkurugenzi wa Mifuko ya Uwezeshaji wa NEEC. Edwin Chrissant amesema kazi moja wapo ya Baraza ni kusimamia, kuratibu na kufuatilia shughuli zote za kiuchumi ikiwemo ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji hivyo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ni fursa kubwa ambayo Watanzania wanaihitaji.

“Ujenzi wa mradi huu ni moja ya miradi mikubwa kufanyika nchini ambao utagharimu jumla ya shilingi trilioni 8 na bomba hili litakuwa na urefu wa Kilomita 1445 kati ya hizo kilomita 1149 sawa na asilimia 80 ziko Tanzania hivyo watanzania wakiwemo wale walio karibu na sehemu za ujenzi huo wanahamasishwa kujiunga na ATOGS ili kujengewa uwezo wa jinsi ya kutumia fursa hizo ”alisema Chrissant.

[caption id="attachment_8194" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Mifuko ya Uwezeshaji toka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bw. Edwin Chrissant akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) fursa zilizopo za uwekezaji kupitia mifuko ya hifadhi, katikati ni Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania (ATOGS) Abdulsamad Abdulrahim na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo. (Picha na: Eliphace Marwa)[/caption]

Chrissant alifafanua kuwa bomba hilo ambalo litapita katika mikoa nane ikiwemo ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara pamoja na Tang,ujenzi wake utachukua kati ya miezi 24 hadi 36 hadi kukamilika.

Nae, Makamu Mwenyekiti wa ATOGS, Abdulsamad Abdulrahim ameihakikishia Serikali kuwa watoa huduma waliopo nchini wameonesha uwezo na utayari wa kutoa huduma nyingi za kitaalam na nyinginezo zilizopo katika mnyororo wa ongezeko la thamani zitakazohitajika wakati wa ujenzi wa bomba la mafuta.

”Inatia moyo kwamba ushiriki wa watoa huduma wa Tanzania katika Sekta hiyo unapewa nguvu kisheria pia tunaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuthibitisha msimamo wake wa kutaka kuona Watanzania wananufaika na fursa za sekta hii jambo linaloleta matumaini mapya kwa jumuiya yetu,” alisema Abdulrahim.

ATOGS ilianzishwa kama chombo cha juu nchini kinachowakilisha na kusimamia maslahi ya wadau na makampuni yanayotoa huduma katika sekta ya mafuta na gesi nchini.

Uanzishwaji wa Jumuiya hiyo ulizingatia uwepo wa fursa zitokanazo na rasilimali za mafuta na gesi zikiwemo za ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta pamoja na mipango iliyopo ya kusambaza gesi katika miji mikubwa nchini.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi