Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wachimbaji Wadogo Kunufaika na Vituo vya Umahiri
Jul 09, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33426" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Madini Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichan) wakati wa kusaini mikataba mitatu ya ujenzi wa vituo saba vya umahiri pamoja na jengo la mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika chuo cha Madini Dodoma.Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Madini Mhe.Stanslaus Nyongo,Kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof Simon Msanjila na Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi-SUMA JKT Mhandisi Morgan Nyonyi.[/caption]

Frank Mvungi

Kuhakikisha wachimbaji wadogo wa madini wanaendelea kunufaika na rasilimali za madini, Wizara ya Madini imesaini hati ya makubaliano na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) kujenga vituo vha umahiri kwenye mikoa saba nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuweka saini hati ya makubaliano ya ujenzi wa jengo la Chuo cha Madini na vituo hivyo saba, Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki amesema mradi huo utatekelezwa na SUMA JKT na unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 11 na vituo hivyo vya umahiri vitajengwa kwenye mikoa ya Katavi, Tanga, Kagera, Simiyu, Mbeya, Mara na Ruvuma.

Waziri Kairuki ameeleza kuwa vituo hivyo vitakuwa na vyumba vya madarasa, mikutano, maktaba, karakana na maabara zitakazotumika kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo.

[caption id="attachment_33427" align="aligncenter" width="800"] Katibu Mkuu Wizara Wizara ya Madini Prof Simon Msanjila(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi-SUMA JKT Mhandisi Morgan Nyonyi wakibadilishana mkataba wa ujenzi wa vituo saba vya umahiri pamoja na jengo la mafunzo kwa wachimbaji wadogo na vitakavyojengwa katika chuo cha Madini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33428" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Madini Mhe.Angellah Kairuki na Naibu Waziri wake Mhe. Stanslaus Nyongo wakishuhudia utiaji saini mikataba mitatu ya ujenzi wa vituo saba vya umahiri pamoja na jengo la mafunzo kwa wachimbaji wadogo vitakavyojengwa katika chuo cha Madini Dodoma.Wanaotia saini ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof Simon Msanjila na Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi-SUMA JKT Mhandisi Morgan Nyonyi. Picha na Daudi Manongi[/caption] Akieleza umuhimu wa vituo hivyo Waziri Kairuki amesema vitasaidia kutoa mafunzo ya jiolojia hususan katika utafiti wa madini, uchenjuaji wa madini kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira. Faida zingine ni pamoja na mafunzo ya biashara ya madini, usalama na afya sehemu za kazi na utunzaji wa mazingira kwenye migodi ya wachimbaji wadogo. Kuongeza mchango wa wanawake kwenye sekta ya madini nchini mheshimiwa Kairuki amesema serikali itafanya maboresho ya miundo mbinu ya chuo hicho ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli zinazofanywa na chama cha Wachimbaji Madini Wanawake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa bajeti  kwa mwaka 2018/2019. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji, Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi kutoka SUMA JKT, mhandisi Morgan Nyoni amemuhakikishia Waziri Kairuki kuwa ujenzi wa vituo hivyo utazingatia ubora na viwango kwa sababu nia na dhamira ya SUMA JKT ni kufanya kazi yenye weledi kwa maslahi ya taifa. Kwa mujibu wa mkataba ujenzi wa vituo hivyo unatarajia kukamilika ifikapo Disemba 2018 na unatekelezwa kupitia mradi wa Usimamizi endelevu wa rasilimali madini (Sustainable Management of Mineral Resources Project- SMMRP)             “

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi