[caption id="attachment_6040" align="aligncenter" width="750"] Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mhe. Anna Makinda, akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga (kushoto) wakati alipotembelea Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) ili kujionea kazi zinazofanywa na mfuko huo pamoja na Taasisi mbalimbali wakiwemo wajasiriamali wadogo.[/caption] [caption id="attachment_6043" align="aligncenter" width="750"] Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mhe. Anna Makinda, akimkabidhi Kadi ya Bima ya Afya mmoja wa watoto waliosajiliwa na mfuko huo ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wananchi kujiunga na NHIF.[/caption]
Na Frank Mvungi
Vituo vya afya vinavyo milikiwa na Serikali vimetakiwa kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ili kusogeza huduma za afya karibu na wananhi.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF ambaye pia ni Spika Mstaafu, Anna Makinda, baada ya kutembelea Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere.
Makinda alieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anafikiwa na huduma ya Bima ya Afya kupitia mfuko huo.
“Mfuko wa Bima ya Afya haufanyi biashara na niseme tu kwamba tunachokifanya ni kutoa huduma kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kuhakikisha kuwa huduma za afya hapa nchini zinaimarika na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi”, alieleza Makinda.
Alieleza kuwa Mfuko huo umekuwa ukitoa mikopo ya vifaa tiba, dawa pamoja na nyenzo nyingine kusaidia kuboresha huduma za afya hasa katika hospitali na vituo vya kutolea huduma za afya vilicyosajiliwa na mfuko huo.
Pia mama Makinda amewaasa Watanzania kujiunga NHIF ili wanufaike na huduma na pia kuepuka usumbufu pale wanapougua kwani kwa kufanya hivyo watakuwa pia wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga alieleza kuwa mpaka sasa kuna jumla ya vituo vya afya 6,998 nchi nzima ambayo vinatoa huduma za afya kupitia NHIF na kwamba katika kipindi hiki cha maonesho ya Saba Saba pekee Mfuko huo umesajili watoto 1,450 kupata huduma za afya.
Mfuko wa Bima ya Afya umekuwa ukiwahahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko huo ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu pale wanapougua.