Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Viongozi wa Umma Wakumbushwa Kuwasilisha Fomu za Tamko la Mali Kabla ya Mwaka Kuisha
Dec 27, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_25680" align="aligncenter" width="750"] Kamishna wa Secretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu tarehe ya mwisho ya kupokea fomu ya tamko la mali za Viongozi leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu anayeshughulikia Maadili ya Viongozi wa Kisiasi Waziri Kipacha. Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa wamewasilisha fomu za tamko la mali zao kabla ya tarehe 31 Desemba 2017.[/caption]

Na: Jacquiline Mrisho

Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amewahimiza Viongozi wa Umma kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu za tamko la rasilimali na madeni kabla ya Disemba 31 mwaka huu.

Ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inayomtaka kiongozi wa umma kupeleka tamko kwa maandishi lililo katika hati rasmi linaloorodhesha mali au rasilimali za kiongozi na familia yake kwa Kamishna wa Maadili kila mwisho wa mwaka.

[caption id="attachment_25681" align="aligncenter" width="750"] Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu tarehe ya mwisho ya kupokea fomu za tamko la mali za viongozi leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu anayeshughulikia Maadili ya Viongozi wa Siasi Waziri Kipacha na Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Sekretarieti hiyo Filotheus Manula. Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa wamewasilisha fomu za tamko la mali zao kabla ya tarehe 31 Desemba 2017.[/caption] [caption id="attachment_25682" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Filotheus Manula akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu adhabu anazoweza kupewa kiongozi ambaye atachelewesha kuwasilisha Tamko la maandishi la mali zake leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela. Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa wamewasilisha fomu za tamko la mali zao kabla ya tarehe 31 Desemba 2017.[/caption]

Jaji Mstaafu Nsekela amesema kuwa fomu za tamko hilo zinapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya maadili ambayo ni www.ethicssecretariat.go.tz hivyo ametoa wito kwa viongozi ambao hadi sasa hawajapata fomu kutumia tovuti hiyo kupata fomu kwa urahisi.

“Kwa kuzingatia kifungu cha 9 (1) (a) na (c) cha Sheria na Maadili ya Viongozi wa Umma, viongozi wapya wanaochaguliwa au kuteuliwa wanatakiwa kujaza fomu hizi ndani ya siku thelathini baada ya kupewa wadhifa fulani pia anapofika mwisho wa kutumikia wadhifa huo anapaswa kujaza fomu na kuzirejesha katika ofisi yetu,”alisema Jaji Mstaafu Nsekela.

[caption id="attachment_25683" align="aligncenter" width="750"] Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela (katikati) akipitia sheria ya Maadili ya Viongozi alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu tarehe ya mwisho ya kupokea fomu ya tamko la mali za viongozi leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu anayeshughulikia Maadili ya Viongozi wa Siasi Waziri Kipacha na Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Sekretarieti hiyo Filotheus Manula. Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa wamewasilisha fomu za tamko la mali zao kabla ya tarehe 31 Desemba 2017.[/caption] [caption id="attachment_25684" align="aligncenter" width="750"] Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu tarehe ya mwisho ya kupokea fomu za tamko la mali za viongozi leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu anayeshughulikia Maadili ya Viongozi wa Kisiasa, Waziri Kipacha, Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Sekretarieti hiyo Filotheus Manula na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Rodney Thadeus (kulia).Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa wamewasilisha fomu za tamko la mali zao kabla ya tarehe 31 Desemba 2017.[/caption]

Jaji Mstaafu Nsekela amefafanua kuwa fomu hizo zinatakiwa kuwasilishwa katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma zilizopo Jijini Dar es Salaam au katika ofisi zao za Kanda zilizopo katika Mikoa ya Dodoma, Mwanza, Arusha, Mtwara, Tabora, Pwani na Mbeya.

Kwa upande wake Afisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti hiyo, Filotheus Manula amesema kuwa kujaza fomu hizo ni takwa la kikatiba hivyo Viongozi wa Umma wahakikishe wanajaza fomu hizo bila kudanganya.

“Ni kosa kwa mujibu wa Kifungu cha 15(c) cha Sheria za Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kiongozi kushindwa kutoa tamko bila sababu ya msingi kwani sheria hizi hazimzuii kiongozi kumiliki au kuwa na mali nyingi bali mali hizo zinatakiwa kutolewa maelezo ya chanzo cha upatikanaji wake,” alisema Manula.

[caption id="attachment_25685" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano baina yao na Kamishna wa Maadili alipokua akitoa ufafanuzi kuhusu mwisho wa kupokea Matamko ya Mali za Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa wamewasilisha fomu za tamko la mali zao kabla ya tarehe 31 Desemba 2017.(Picha na: Frank Shija)[/caption]

Aidha, Manula amefafanua kuwa kosa hilo linaweza kumpelekea muhusika kuonywa au kupewa adhabu ya kushushwa cheo, kusimamishwa, kufukuzwa kazi pamoja na kupelekwa Mahakamani.

Vile vile Manula amesema kuwa kwa sasa hali ya uadilifu kwa Viongozi wa Umma inaridhisha kwani ukiukwaji wa maadili umepungua kwa kiasi kikubwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi