Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

VIJANA WAHAMASISHWA KUJIUNGA NA KILIMO CHA MBOGAMBOGA,MATUNDA NA NAFAKA.
Apr 25, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_400" align="alignnone" width="712"] Mwenyekiti wa Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga Wilaya ya Temeke, Joseph Kunguru (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya kuwahamasisha Vijana kujihusisha na kilimo cha kisasa cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Buza, Manispaa ya Temeke, James Raphael Mkude na Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo Waziri Pembe Waziri.[/caption] [caption id="attachment_401" align="aligncenter" width="338"] Diwani wa Kata ya Buza Manispaa ya Temeke James Raphael Mkude akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana Kampeni ya kuwahamasisha vijana kujihusisha na kilimo cha kisasa cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_402" align="aligncenter" width="630"] Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia kwa umakini mkutano baina yao na viongozi wa Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Husna Saidi[/caption]

Na Nuru Juma na Husna Saidi-MAELEZO

Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga, Matunda na Nafaka umeanzisha Kampeni ya Kijana Inuka na Kilimo cha Mbogamboga na Matunda kwa lengo la kuepukana na kilimo cha mvua na vijana waweze kujiajiri wenyewe.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Wilaya ya Temeke Joseph Kunguru alipokutana na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Kunguru alisema kuwa kilimo hicho ni kilimo biashara  na kinahitaji maji na miundombinu ya uhakika ili kuwafanya wananchi kulima kilimo chenye tija badala ya kulima kwa kutegemea mvua.

“Kilimo hiki kinaonekana ni kilimo ghari sana kwani ujenzi wa Green House unaonekana ni kilimo cha watu wenye pesa lakini ukweli ni kwamba wananchi wakiungana pamoja katika kilimo hiki wanaweza kufanikiwa badala ya kulima kwa kutegemea mvua,” alisema Kunguru.

Aidha alisema kuwa vijana wengi mtaani hawana ajira hivyo viongozi kupitia kampeni hii watumie fursa hiyo kuwaelimisha kuhusiana na kilimo hiki cha umwagiliaji ili waweze kujiajiri wenyewe.

Umoja huo wa kilimo cha Mbogamboga na Matunda na Nafaka umesajiliwa kisheria na ulianza na wanachama 17 mpaka sasa wapo 100 ila wanachama hai wapo 74 hivyo wanawasihi wananchi waendelee kujitokeza kujiunga.

Kwa upande wake mmoja wa wanakikundi hicho Sifa Karuka alisema alihamasika kujiunga na kikundi hicho baada ya kupata taarifa kuhusu kilimo hicho cha kisasa  licha ya kuwa na shughuli zake binafsi hivyo anawasihi wakinamama na wasichana wajitokeze kwa wingi ili waweze kujiendeleza kiuchumi.

Nae Diwani wa Kata ya Buza James Raphael Mkude aliwahamasisha madiwani wenzie kuweza kuunda vikundi kama hivyo katika kata zao ili wananchi wao hasa vijana wasiokuwa na ajira waweze kujikwamua kiuchumi.

Kikundi hicho kimeiomba Serikali kupitia Maofisa Ugani kutoa mafunzo kwa vijana ambao hawana ajira kuhusiana nakilimo hicho ili kupunguza ukosefu wa ajira kwa kujitegemea wao wenyewe.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi