Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Uyui Yajivunia Mafanikio ya Miaka 4 ya Serikali ya Awamu Tano
Nov 29, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_49477" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Msuya akisisitiza kuhusu mikakati yake ya kuhakikisha wanafikia maendeleo endelevu kupitia miradi inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi.[/caption]

Na mwandishi Wetu

Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kuleta mageuzi katika sekta ya Afya, Maji, Elimu na sekta nyingine zinazolenga kuwainua wananchi kiuchumi katika Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora.

Akizungumza katika mahojiano maalum kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka 4 ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Gift Msuya amesema kuwa moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa Hospitali ya wilaya  uliogharimu shilingi bilioni 1.6 na ujenzi umefikia asilimia 95 na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Novemba, 2019.

 “ Ujenzi wa Hospitali ya wilaya  umeenda sambamba na kujengwa kwa Vituo vya Afya kama kile cha  Upuge kilichogharimu shilingi milioni 500,000 na kimekamilika na kuanza kutoa huduma tayari wagonjwa 62 wamefanyiwa upasuaji katika kituo hiki,” alisisitiza Msuya

Akifafanua amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 400 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Igalula na ujenzi umefikia asilimia 95 na kinaratajia kukamilika hivi karibuni ili kiweze kuanza kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Katika sekta ya Elimu, wilaya hiyo imefanikiwa kujenga Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Ubora wa Elimu Uyui iliyogharimu milioni 130  na imekamilika kwa asilimia 100 hali itakayochangia kukuza kiwango cha elimu wilayani humo.

Miradi mingine ni ile ya maji ambayo imegharimu zaidi ya bilioni 3 zizilotolewa ili kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo kwa lengo la kuwezesha wananchi kupata huduma bora zaidi ya maji safi na salama.

Ujenzi wa madarasa ya EQUIP na lipa kadiri ya matokeo (EP4R) umegharimu zaidi ya bilioni 1.5 na  kumewezesha kupungua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika wilaya hiyo.

Akizungumzia miradi iliyotekelezwa kwa kushirikiana na wadau katika sekta za Afya na Maji, Mhe. Msuya amesema kuwa  imegharimu takriban bilioni 1.1 na hivyo kutoa mchango katika kuleta ustawi wa wananchi.

Wilaya ya Uyui mkoani Tabora ni moja ya wilaya zilizopiga hatua katika kukuza sekta ya Kilimo ili kuwainua wananchi kiuchumi na kujenga uchumi jumuishi.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi