Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Uwanja wa 'AFCON' Arusha Utakidhi Viwango Kimataifa-Dkt. Nchemba
Apr 17, 2026
Uwanja wa 'AFCON' Arusha Utakidhi Viwango Kimataifa-Dkt. Nchemba
Waziri MkuuMhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akikagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu unaojengwa mkoani Arusha kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027.
Na Mwandishi Wetu - Arusha

Waziri MkuuMhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Aprili 17, 2026 amekagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu unaojengwa mkoani Arusha kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027.

Uwanja huo unatarajiwa kuwa miongoni mwa miundombinu muhimu itakayotumika wakati wa mashindano hayo yatakayofanyika kwa pamoja katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Dkt. Nchemba amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyokidhi mahitaji ya kimataifa, ili kuiwezesha Tanzania kuwa mwenyeji bora wa mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika.

Amesema Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya kimkakati ili kuhakikisha nchi inanufaika kikamilifu na fursa zinazotokana na mashindano ya AFCON 2027.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi