[caption id="attachment_45365" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface akisaini mkataba wa ushirikiano kati ya MOI na Taasisi ya BMVSS Jaipur ya India.[/caption]
Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) leo isimden numara sorgulama tarehe 16/07/2019 imeingia mkataba wa ushrikiano wa Mafunzo, kubadilishana wataalamu pamoja na utaalamu na Taasisi ya BMVSS Jaipur ya nchini India ambayo iliratibu kambi ya utoaji miguu bandia bure kwa watu zaidi ya 551.
Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface pamoja na muanzilishi na mlezi wa Taasisi ya BMVSS Dkt. D.R Mehta ambapo zoezi hilo la kutia saini limeshudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya MOI Prof. Charles Mkonyi pamoja na Mkurugenzi wa uendeshaji na ushirikiano wa kimataifa wa BMVSS Bw. Satich MehtaSS
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema mkataba huu utasaidia kuwajengea uwezo wataalamu wa MOI ambapo watapata fursa ya kupata mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi katika Taasisi ya BMVSS.
“Mkataba huu utasaidia sana kwani lengo letu ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma hizi za viungo saidizi na bandia kwa ubora wa hali ya juu ili kuwasaidia watanzania hususani wa kipato cha chini ili waweze kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.” Alisema Dkt Boniface
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji na Uhusiano wa Kimataifa BMVSS Bw. Satich Mehta amesema BMVSS itatoa fursa kwa wataalamu wa MOI kupata mafunzo nchini India bila gharama yoyote.
“Tutatoa fursa kwa wataalamu wa MOI kuja kujifunza kwa miezi miwili au zaidi ,lengo letu ni kuhakikisha ujuzi zaidi unapatikana hapa MOI na wananchi wengi zaidi wananufaika hususani wale wa kipato cha chini” alisema Bw Mehta.
Taasisi ya MOI imekua ikianzisha ushirikiano na Taasisi Mbalimbali za ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuendelea kuboresha
huduma zake.
[caption id="attachment_45366" align="aligncenter" width="900"]