Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

UNDP yachangia Milioni 110 Huduma ya Maji Kikwajuni Zanzibar
Jun 23, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_4219" align="aligncenter" width="750"] Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akifunga bomba la maji katika moja ya maeneo ambayo Mradi wa Maji Kikwajuni ushakamilika. UNDP wameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika maeneo yote ya jimbo hilo.Picha na Abubakari Akida.[/caption]

Na Abubakari Akida-Zanzibar

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limechangia kiasi cha shilingi 110 milioni katika kuwezesha huduma za maji kwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni kupitia Mradi wa Maji Kikwajuni uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein miaka miwili iliyopita.

Akizungumza na wananchi wa jimbo hilo baada ya kutembelea vituo na vyanzo vya mradi huo vya Migombani na Kilimani, Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP, Alvaro Rodriguez alisema lengo lao ni kuona mradi huo unakamilika ili KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI.

“Nimeridhishwa na maendeleo ya mradi unaotarajiwa kutoa huduma kwa wakazi zaidi ya 10,000 wa jimbo hili. UNDP inachangia kiasi cha shilingi milioni 110 ili mradi huo uweze kukamilika na wananchi wapate huduma ya maji,” alieleza.

[caption id="attachment_4220" align="aligncenter" width="750"] Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akisadiana na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa jimbo hilo wakati wa ziara ya ukaguzi wa maeneo ulikopitia Mradi wa Maji Kikwajuni ambapo UNDP wameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 kufanikisha kukamilika kwa mradi huo.[/caption] [caption id="attachment_4221" align="aligncenter" width="750"] Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Visiwani Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa Kikwajuni Mao, katika mkutano huo aliongozana na Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Salama Abood Talib. UNDP wameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha Mradi wa maji katika jimbo hilo. (Picha na Abubakari Akida[/caption]

Akizungumza kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, Mhe. Salama Abood Talib, alisema lengo la serikali ni kuhakikisha inashirikisha wadau mbalimbali katika kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa wananchi wa maeneo mbalimbali visiwani humo na amemshukuru mwakilishi wa UNDP kwa msaada waliotoa katika kumalizia mradi huo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni amesema mradi huo una awamu tatu huku awamu mbili zikiwa  zishakamilika na wapo katika awamu ya mwisho ya kukamilisha mradi huo.

Akizunguma kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, Ahmed Said Makame alisema jimbo la Kikwajuni limekua na changamoto ya huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo na ameshukuru kuwa mradi huo utakapo kamilika utakuwa umeondoka tatizo la maji katika eneo hilo.

Mradi wa Maji Kikwajuni unakadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 344,000,000 ambapo awamu ya kwanza na ya pili iligharamiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mbunge wa Jimbo hilo, michango ya wananchi na Serikali ya Japan.

Mradi huo utakapokamilika utanufaisha wakazi zaidi ya 10,000 wa jimbo la Kikwajuni, visiwani Zanzibar.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi