Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ujenzi wa Viwanja vya Michezo ni Jukumu la Serikali na Wadau: Mhe. Gekul
Sep 16, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Shamimu Nyaki

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul amesema ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya michezo ni jukumu la Serikali Kuu, Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Taasisi, Mashirika ya Umma na Wadau wa michezo.

Ameyasema hayo leo Septemba 16, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mhe. Shaban Omari Shekilindi (Lushoto) aliyeuliza Je ni lini Serikali itajenga Uwanja wa Michezo katika Mji wa Lushoto.

Napenda kutumia nafasi hii, kuzikumbusha Halmashauri nchini ikiwemo Halmashauri ya Lushoto, kuzingatia matakwa ya Sera ya Michezo kwa kutenga fedha  kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kukarabati na kujenga miundombinu ya michezo", amesema Mhe.Gekul.

Mhe.Gekul ameeleza kuwa Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995 Ibara 7 inaeleza kuwa, jukumu la ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya michezo ni jukumu la watu wote na mazingira ya kuwekeza yameainishwa kwa uwazi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi