Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ujenzi wa Majengo ya NEC Kukamilika Ndani ya Muda Uliopangwa.
Oct 19, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_20507" align="aligncenter" width="750"] Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R), Simistocles Kaijage, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Bw. Ramadhan Kailima na Mhandisi kutoka Wakala wa Majengo (TBA), Bw. Yohana Mashausi wakiwaongoza makamishna wa NEC kutembelea eneo la mradi wa ujenzi wa majengo ya ofisi za NEC jana. Mradi huo unafanyika katika eneo la Njedengwa Mjini Dodoma.[/caption]

Na Mwandishi wa NEC- Dodoma

Makamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wametembelea eneo la Njedengwa Mjini Dodoma yanapojengwa majengo ya makao makuu ya NEC na kuelezea kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo, ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya tano chini ya Dkt.John Pombe Magufuli za kuhamishia Makao Makuu ya nchi Mjini Dodoma.

Akizingumza mara baada ya ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji (R) Semistocles Kaijage, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Bw. Ramadhan Kailima alisema kwamba maendeleo ya ujenzi yanaridhisha na ujenzi utakamilika kwa muda uliopangwa.

[caption id="attachment_20509" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R), Simistocles Kaijage (wa pili kulia) akifurahia jambo na Mhandisi kutoka Wakala wa Majengo (TBA), Bw. Yohana Mashausi (kulia) baada ya kupewa maelezo ya mradi wa ujenzi wa majengo ya ofisi za NEC jana wakati makamishana wa NEC walipotemdelea mradi huo. Mradi huo unafanyika katika eneo la Njedengwa Mjini Dodoma na unatarajiwa kukamilika mwakani.[/caption] Bw. Kailima amesema kwamba awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo ambao unajumuisha majengo matatu utakamilika mwezi Julai, mwakani.

“Mradi huu una awamu mbili za ujenzi lakini utatoa majengo makubwa matatu, jengo la kwanza ni jengo kubwa la ofisi litakua na ghorofa nane, la pili ni jengo la ukumbi wa kutangazia matokea ambao utakua na uwezo wa kuchukua watu 800, uchaguzi Mkuu ujao wa 2020 tunatarajia kutangaza matokeo kwenye ukumbi huu na pia kuna jengo la maghala ya kuhifadhia vifaa vya uchaguzi,” amesema Bw. Kailima.

Aliongeza kusema “Mradi huu unakwenda vizuri kwa sababu gharama yake ni takribani shilingi bilioni 13, awamu ya kwanza itagharimu bilioni 11/- ambayo itahusisha ujenzi wa jengo la ofisi, pia itajumuisha ujenzi wa sehemu ya jengo la kituo cha kutangazia matokeo na maghala. Awamu ya pili ambayo itagharimu bilioni 2/- itakua imekamilika mwaka 2018. Kuanzia mwenzi Agosti 2018 Tume tutaanza kuhamia Dodoma,” amesema.

[caption id="attachment_20510" align="aligncenter" width="750"] Kutoka kushoto ni Mhandisi kutoka Wakala wa Majengo (TBA), Bw. Yohana Mashausi akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa makamishna wa tume hiyo walioongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R), Simistocles Kaijage, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Bw. Ramadhan Kailima na Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid. Ujenzi huo unaoendelea katika eneo la Njedengwa Mjini Dodoma unatarajiwa kukamilika mwakani. (Picha na Abdulwakil Saiboko).[/caption]

Akizungumzia suala la bajeti ya ujenzi wa majengo hayo, Bw. Kailima amesema fedha zipo na zitakua zikitolewa kadri zitakavyohitajika.

Mwanzoni akiwatembeza makamishna wa tume kwenye eneo la mradi, Mkandarasi Msimamizi kutoka Wakala wa Majengo (TBA), Mhandisi Yohana Mashausi amesema ujenzi huo umechukua muda mrefu kwenye eneo la msingi kwa kuwa eneo hilo lina ardhi yenye mwamba mgumu sana.

Mhandisi Mashausi amesema kwamba TBA pia imechukua tahadhari kubwa katika ujenzi wa msingi imara kwa kuzingatia hali ya kijogirafia ya Dodoma ambako kuna hatari ya kukumbwa na matetemeko ya ardhi.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi