Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tumieni Gesi Badala ya Kuni, Mkaa - Dkt. Biteko
Apr 29, 2024
Tumieni Gesi Badala ya Kuni, Mkaa - Dkt. Biteko
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Aprili 29, 2024 amefungua Mkutano Mkuu wa 13 wa Mwaka wa Kitaaluma wa Jukwaa la Wahariri Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa St. Gasper jijini Dodoma na kuwataka wanahabari wajisimamie na kuilinda taaluma ya habari.
Na Jonas Kamaleki- Dodoma

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kutumia gesi na kuacha matumizi ya kuni na mkaa ili kuokoa mazingira.

"Tunataka mama wa kijijini atumie gesi na aachane na matumizi ya kuni na mkaa. Madhara ya kuni ni makubwa na yanasababisha macho kuwa mekundu mpaka katika baadhi ya mikoa watu wanaanza kupewa tuhuma nyingine (uchawi)," alisema Dkt. Biteko.

Aidha, amewaomba  wahariri waunge mkono juhudi za serikali za kuhifadhi misitu na kuunga mkono nishati ya kupikia.

"Sisi hapa Tanzania tuna gesi safi. Serikali inahamasisha matumizi ya gesi ili kuepukana na madhara ya nishati nyingine. Tumepunguza urasimu katika kutoa leseni ya vituo vya gesi asilia kwa ajili ya magari yanayotumia gesi," aliongeza Dkt. Biteko.

Aidha, Dkt. Biteko alivitaka vyombo vya habari vilinde tamaduni za watanzania na kuwafanya wajivunie kuwa watanzania.

Kwa upande wake,
Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
alisema kuwa ushirikiano wa wanahabari ni mkubwa mno. Kuna matukio mbalimbali ambayo wanahabari tumeshirikiana nao ikiwamo maadhimisho ya miaka 60 ya muungano

Waandishi wanaandika habari zao bila woga kama ipo basi ni hofu tu waliyojijengea, alisema Mhe. Nape.

"Nawataka wanahabari zingatieni sheria, zingatieni kanuni, zingatieni maadili, na zingatieni busara," alisisitiza Mhe. Nape.

Naye, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile ameipongeza Idara ya Habari (Maelezo) kwa kuanzisha mikutano ya waandishi wa habari na Taasisi za serikali ambayo inatoa fursa kwa waandishi wa habari kuwa na wigo mpana wa utendaji wa Serikali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi