Na Mwandishi Wetu - MAELEZO
Shilingi trilioni 70 zinatarajiwa kutumika kutekeleza mradi wa kusindika na kuchakata gesi asilia (LNG) mkoani Lindi.
Hayo yamesemwa leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba katika hafla ya uwekaji saini wa makubaliano ya awali ya mkataba wa nchi hodhi wa mradi huo.
"Utekelezaji wa
Mradi huu unakadiriwa kugharimu zaidi ya Dola za Marekani, Bilioni
thelathini sawa na takribani Shilingi trilioni Sabini," ameeleza Waziri Makamba.
Pamoja na hilo, Mhe. Makamba amezipongeza kampuni za Equinor, Shell na wabia wao kwa
ushirikiano wanaoendelea kuipatia Serikali katika kuhakikisha kuwa mradi
huu unafanyika kwa maslahi ya Taifa na Wawekezaji.