Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo (kulia), akielezea masuala mbalimbali ya shirika hilo, katika kujiimarisha kimataifa, ambayo waliyatoa katika mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Mashirika ya Posta duniani (UPU). Wa pili kulia ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe na kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika Macrice Mbodo. Baadhi ya viongozi waandamizi wa shirika hilo, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa kwa waandishi wa habari na Mwenyekiti wa Bodi, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo leo, jijini Dar es Salaam. Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mipango ya kujizatiti kimataifa kwa shirika lake hilo. Pia Mwenyekiti wa Bodi kabla ya mkutano huo alizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo, jijini Dar es Salaam jana, ambapo, aliwaelezea yaliyojiri katika mkutano huo wa kimataifa wa Umoja wa Mashirika ya Posta duniani (UPU). Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakimsikiliza Mwenyekiti wao wa bodi, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo, alipozungumza nao.