Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Toeni Elimu ya Kulima Kitaalamu kwa Mazao Yote-Mwanri.
Dec 13, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na: Tiganya Vincent

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imewaagiza Maofisa Ugani kuhakikisha watoa elimu kwa wakulima kulima mazao yote kitaaalamu na kwa kuzingatia kanuni za kilimo bora ili kuwaongezea uzalishaji wa mazao mbalimbali na tija.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wilayani Igunga baada ya kujionea mazao mbalimbali yakiwemo mahindi na choroko zikiwa zimepandwa bila kuzingatia vipimo vinavyotakiwa kitaalamu.

Alisema kuwa kanuni za kilimo bora haziwezi kuwa kwa ajili ya mazao ya biashara ya tumbaku na  pamba pekee bali ni lazima sisitizwe kutumika katika kwa mazao yote yanalomwa mkoani humo ili uzalishaji uongezeke na Halmashauri ziwe kupata kodi zaidi.

Mwanri kuwa kitendo cha Maofisa Ugani kuwaacha wakulima kuendelea kulima kama walivyozoea bila kuzingatia kanuni za kilimo bora kinaoonyesha kuwa watumishi hao hawajatimiza majukumu yao vema.

Alisema kuwa kazi kubwa ya Maofisa Ugani ni kumsaidia mkulima ili haweze kuondokana na kilimo duni na hatimaye alime kisasa kwa ajili ya maendeleo yake na Taifa kwa ujumla.

Mwanri alisema kuwa wakulima wamekuwa wakijutumia kulima maeneo makubwa lakini mavuno hayalingani na nguvu walizotumia kwa sababu ya kukosa ushauri wa kitaalamu wa kuwahimiza ujazaji wa mazao katika shamba na matumizi ya mbolea.

Alisema kuwa kuanzia mwakani hatamuonea huruma Afisa Ugani yoyote ambaye kwenye eneo lake la kazi atakuta mkulima amelima bila kuzingatia nkanuni za kilimo bora badala yake amepanda ovyo ovyo katika shamba lake.

Naye Mshauri wa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Modest Kaijage alisema kuwa suala la upandaji kwa kuzingatia vipimo ni kwa ajili ya mazao yote na kuongeza ni vema Maofisa Ugani wote kuanzia ngazi ya vijiji hadi Wilaya kuhakikisha wanahimiza wakulima kuzingatia vipimo ili waweze kupata mazao mengi.

Alisema kuwa wakati muda wa kupanda alizeti umekaribia ni vema Maofisa Ugani wote wakaanza kuhimiza wakulima walime zao hilo kwa vipimo vinavyotakiwa .

Kaijage alisema kuwa hatua hiyo itawasaidia wakulima kulima eneo dogo lakini ambalo litakuwa na mimea mingi iliyopandwa katika umbali unaotakiwa kitaalamu ambalo litampa mkulima mavuno mazuri

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi