[caption id="attachment_37659" align="aligncenter" width="750"] Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima mkoa wa Dodoma Bw. Habibu Muyula akisisitiza jambo wakati wa ziara ya ujumbe wa Taasisi hiyo Wilayani Kongwa mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo ya elimu juu ya kuzuia ndoa za kulazimishwa za utotoni katika Wilaya hiyo leo, ambapo mradi huo unatekelezwa katika Wilaya hiyo na ile ya Bahi kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu wazima.[/caption]
Na; Mwandishi Wetu
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kwa kushirikiana na Shirika la Elimu ya Jumuiya ya Madola kuendelea kuwawezesha wasichana waliokosa elimu katika mfumo rasmi kutokana na ndoa za kulazimishwa za utotoni kupata stadi za maisha ili waweze kujitegemea.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya mradi wa GIRLS Inspire katika Wilaya ya Kongwa, Mkufunzi mkazi wa Taasisi hiyo mkoani Dodoma Bw. Habibu Muyula amesem kuwa dhamira yao ni kuona kundi hilo la wasichana waliokosa elimu katika mfumo rasmi linajikwamua kielimu na kiuchumi kupitia mafunzo waliyopata, yakielenga kuwajengea uwezo wa kujitambua, stadi za uzalishaji na ubunifu kwa lengo la kuwakumboa kifikra na kiuchumi.
"Tumewajengea uwezo mabinti hawa ambao kutokana na mimba za utotoni walishindwa kuendelea na masomo, hapa Kongwa tayari wameshawezeshwa kuanza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo batiki,sabuni na kusindika bidhaa"; Alisisitiza Muyula.
[caption id="attachment_37660" align="aligncenter" width="863"] Afisa Elimu ya Watu Wazima Wilaya ya Kongwa Bi. Jane Lutego akiwasisitiza wahitimu wa mafunzo ya mradi wa elimu juu ya kuzuia ndoa za kulazimishwa za utotoni katika Wilaya hiyo kuzingatia stadi walizopata katika kujiletea maendeleo kwa kukuza vikundi vya uzalishaji, hayo yamejiri leo mkoani Dodoma ambapo mradi huo unatekelezwa katika Wilaya hiyo na ile ya Bahi kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu wazima.[/caption]Akifafanua amesema kuwa taratibu za kusajili vikundi hivyo zinaendelea ili kuweka mazingira yakuviwezesha kupitia Halmashauri husika na wadau mbalimbali.
Kwa upande wake, Afisa Elimu ya Watu Wazima wa Wilaya ya Kongwa Bi. Jane Lutego amesema kuwa mafunzo hayo ni ukombozi kwa wasichana hao waliokosa elimu katika mfumo rasmi na jambo la muhimu ni wao kujitambua na kutumia elimu hiyo katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.
"Nafurahi kuona kuwa wasichana hawa sasa wanajitambua na wamebahatika kupata elimu ya kuwawezesha kujikomboa kiuchumi na kuisadia jamii, jambo la muhimu ni kuwa na bidii na kujituma katika kuzalisha bidhaa ambazo zitaendana na taaluma mliyopata"; Alisisitiza Lutego.
Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima inaendesha Programu ya kuwawezesha wasichana waliokosa elimu katika mfumo rasmi kuweza kujitegemea kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo Batika na Sabuni katika mkoa wa Dodoma na Rukwa na jumla ya wasichana 1500 wamenufaika na mradi huu.
[caption id="attachment_37661" align="aligncenter" width="750"] Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima mkoa wa Dodoma Bw. Habibu Muyula akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wake pamoja na Afisa Elimu Afisa Elimu ya Watu Wazima Wilaya ya Kongwa Bi. Jane Lutego na Afisa Elimu Vielelezo Bw. Emmanuel Kiula walipowatembelea katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo kwa elimu juu ya kuzuia ndoa za kulazimishwa za utotoni katika Wilaya leo ambapo mradi huo unatekelezwa katika Wilaya hiyo na ile ya Bahi kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu wazima.[/caption] [caption id="attachment_37662" align="aligncenter" width="885"] Muwezeshaji wa Kitaifa wa mradi wa elimu wa kuzuia ndoa za kulazimishwa za utotoni kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Bw. Placid Balige akisisitiza jamabo kwa Afisa Elimu Msingi Bw. Mzenga Twalib Mzenga wakati wa ziara ya ujumbe wa Taasisi hiyo katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ikienga kuhitimishamafunzo ya mradi wa elimu juu ya kuzuia ndoa za kulazimishwa za utotoni katika Wilaya hiyo .[/caption] [caption id="attachment_37663" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya wanufaika wa mafunzo ya mradi wa elimu juu ya kuzuia ndoa za kulazimishwa za utotoni katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakionesha sehemu ya bidhaa wanazozalisha mara baada ya kuhitimu mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoendeshwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yakilenga kuwapa stadi na ujuzi wa kuzalisha bidhaa mbalimbali kupitia katika vikundi vyao.[/caption] [caption id="attachment_37664" align="aligncenter" width="750"] . Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima mkoa wa Dodoma Bw. Habibu Myula akisisitiza jambo kwa Afisa Elimu Vielelezo wa Wilaya ya Kongwa Bw. Emmanuel Kiula hayupo pichani wakati wa ziara ya ya Ujumbe wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima katika Wilaya ya Kongwa leo.[/caption] [caption id="attachment_37665" align="aligncenter" width="891"] Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Kongwa Bw. Mzenga Twalib Mzenga akisistiza jambo kwa ujumbe wa Ujumbe wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima katika Wilaya hiyo leo ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo kwa wahitimu wa mafunzo ya mradi wa elimu wa kuzuia ndoa za kulazimishwa za utotoni katika Wilaya hiyo mapema leo.[/caption] [caption id="attachment_37666" align="aligncenter" width="750"] PIX8. Mtaalamu wa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt. Godfrey Mnubi akisisitiza jambo wakati wa ziara ya ujumbe wa Taasisi hiyo Wilayani Kongwa leo.