Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TBS yawezesha wajasiriamali wadogo kushiriki ujenzi wa uchumi wa viwanda
Oct 20, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37151" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akisisitiza kuhusu hatua iliyochukuliwa na Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo kupata alama ya ubora wa bidhaa wanazozalisha ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa Viwanda kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Shirika hilo, ambapo Serikali inalipa gharama hizo kwa wajasiriamali wadogo, hiyo ilikuwa wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.[/caption]

Na; Frank Mvungi

Serikali  imeendelea kuwezesha wajasiriamali wadogo kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kuwalipia tozo yakupatiwa  alama ya ubora kutoka Shirika la Viwango  Tanzania (TBS)  hali itakayoongeza kasi  ya utekelezaji  wa  azma hiyo ili kukuza uchumi.

Akizungumza  wakati wa Tamasha la Wajasiriamali wanawake linalofanyika Jijini Dodoma na kuwashirikisha wajasiriamali wa ndani na nje ya nchi  wakiwemo  kutoka  nchini Burundi, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika hilo  Bi Roida Andusamile amesema kuwa  dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inawezesha wajasiriamali hao ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora.

“ Serikali kupitia TBS inalipia gharama za kupatiwa alama ya ubora kwenye bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wadogo, wanachopaswa kufanya ni kufuata taratibu za kuwasilisha maombi na mwisho wakikidhi vigezo wanapatiwa hati hiyo”. Alisisitiza Andusamile

Akizungumzia faida za wajasiriamali kudhibitisha ubora wa bidhaa zao, Andusamile amesema kuwa ni pamoja na kukuza soko la wazalishaji  hao ndani na  nje ya nchi ,  pia kukuza viwanda vyao kutoka wajasiriamali wadogo hadi  wajasiriamali wa kati na baadae kuwa wajasiriamali wakubwa.

[caption id="attachment_37152" align="aligncenter" width="900"] Afisa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati Bw. Sileja Lushibika akieleza hatua zinazopaswa kufuatwa na mjasirimali ili kupata alama ya ubora kwa mmoja wa wananchi waliofika katika Banda la Shirika hilo wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.[/caption]

Akifafanua amesema kuwa Shirika hilo limekuwa likitoa elimu kuhusu hatua zinazofuatwa  na mjasiriamali ili kupata hati ya ubora kutoka katika Shirika hilo ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda  hapa nchini.

Aliwataka wananchi kutumia bidhaa zenye ubora na zilizodhibitishwa na Shirika hilo ili kuchochea maedeleo na ukuaji wa sekta ya uzalishaji hasa viwanda vidogo na vile vya kati katika kipindi hiki Serikali inapohamasisha ujenzi wa uchumi wa viwanda.

“ Mjasiriamali anapoanza kuzalisha bidhaa Serikali imetoa kipindi cha mpito ambacho ni miaka 3 ambayo hatatakiwa kulipia ada ya kupatiwa hati ya ubora wa bidhaa anazozalisha kwa kuwa gharama zake zinalipwa na Serikali ikiwa ni hatua ya kuwainua”. Alisisitiza Andusamile.

Aliongeza kuwa baada ya miaka 3 mjasiriamali anapaswa kuanza kulipia hati ya ubora kwa asilimia 25 na baadae asilimia 50 hadi atakapofikisha asilimia 100 lengo likiwa kumjengea uwezo wa kuazalisha kwa ubora na kukidhi vigezo vya ubora.

Kwa upande wake, Afisa Udhibiti Ubora wa Shirika hilo kutoka Kanda ya Kati Dodoma, Bw. Sileja Lushibika amesema kuwa hatua ya kwanza anayopaswa kufuata mjasiriamali ili kupatiwa alama ya ubora ni kuwasilisha maombi kwa mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo na baada ya maombi kupokelewa yatajibiwa ambapo mjasiriamali atatakiwa kuwsilisha taarifa za mfumo wa uzalishaji,malighafi zinazotumika.

Masuala mengine ni taarifa ya safu ya uongozi na mwisho kutakuwa na ukaguzi kabla yakutolewa kwa alama ya ubora ikiwa mjasiriamali atakidhi vigezo.

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekuwa likihamasisha wajasiriamali wadogo kujitokeza na kuwasilisha maombi ya kupatiwa hati ya ubora ili waendane  sambamba na azma ya Serikali kukuza uchumi wa Viwanda.

(Picha na Frank Mvungi)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi