Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TBC Tafuteni Ushauri wa Maeneo kwa Wazawa Kabla ya Kusimika Mitambo Yenu
Dec 29, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_39290" align="aligncenter" width="963"] Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Julianna Shonza akitoa maelekezo ya mambo ya kuzingatia kabla ya kusimika mitambo ya usikivu kwa Meneja wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso (hayupo pichani) leo katika Kijiji cha Kwemashai alipotembelea eneo hilo walilosimika mitambo yao wakati wa ziara yake ya kukagua maeneo iliyoko mitambo ya TBC kwa Kanda ya Kaskazini.[/caption]

Na: Anitha Jonas – WHUSM,Lushoto

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo amewataka  viongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC )kusikiliza ushauri wa wazawa wa maeneo wanayoenda kusimika mitambo yao pale wanapofanya utafiti wa maeneo yatakayofaa kulingana na Jiografia ya eneo husika.

Mheshimiwa Shonza ametoa kauli hiyo leo Wilayani Lushoto alipotembelea eneo lililowekwa mitambo ya TBC iliyoko katika eneo la Kwemashai  kwa lengo la kutaka kubaini changamoto zinazosababisha kutokuwepo kwa usikivu kwa baadhi ya maeneo Wilayani hapo.

[caption id="attachment_39291" align="aligncenter" width="1000"] Mtambo wa kurushia matangazo ya Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) uliyopo katika Kijiji cha Kwemashai Wilayani Lushoto ambapo Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Julianna Shonza alitembelea eneo hilo leo ikiwa ni ziara yake ya kukagua maeneo iliyopo mitambo ya TBC kufuatia changamoto ya usikivu katika maeneo hayo ya Kanda ya Kaskazini.[/caption]

“Changamoto kubwa katika Wilaya hiyo  ya Lushoto ni Jiografia ya eneo hilo kwani inamilima mingi sana kati maeneo yake yote hivyo ni vyema mkashirikiana na Halmashauri katika kuelekezana  eneo abalo itakuwa na mlima mrefu zaidi kushinda yote ambao utawafaa kwakuweza kusimika mtambo wenu utakao rusha matangazo katika maeneo yote ya Wilaya hii,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo aliusisistiza uongozi wa TBC kanda ya Kaskazini kuhakikisha wanafanya utafiti huo haraka na kusimika mitambo hiyo mapema kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha inakamilisha usikivu kwa mikoa iliyoko karibu na maeneo ya mipakani kabla ya mwaka 2020 na ndiyo maana fedha za bajeti ya kuboresha usikivu zinatolewa kila mwaka.

[caption id="attachment_39292" align="aligncenter" width="811"] Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (wapili kulia) akitizama mitambo iliyopo Lushoto, (watatu kulia)Meneja wa Shirika la Utangazaji Taifa Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso akimwonyesha mitambo ya kurushia matangazo ya TBC iliyoko katika eneo la Kijiji cha Kwemashai alipofanya ziara yake aliyoifanya leo ya kukagua maeneo yaliyisimikwa mitambo ya TBC kutokana na kuendelea kuwepo kwa kero ya usikivu katika eneo hilo.[/caption] [caption id="attachment_39293" align="aligncenter" width="768"] Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akikagua Uwanja wa Michezo wa Sabasaba unaomilikiwa na CCM Wilaya ya Lushoto ambao uongozi wa CCM unautafutia mwekezaji wa kuuendeleza leo alipofanya ziara yake ya kikazi leo Wilayani Lushoto.[/caption]

Naye Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Bw.January Lugangika alimwomba Naibu Waziri huyo kuzungumza na uongozi wa TBC kuweza kuwapatia mwandishi kwa Wilaya hiyo ya Lushoto kwani kuhusu suala la ofisi tayari wamekwisha muandalia ipo.

“Tumekuwa tunapata changamoto kubwa ya mwandishi wa TBC kwani inatulazimu kumtumia mwandishi aliyeko Tanga ambaye inamlazimu kusafiri kwa basi kwa mwendo wa masaa matatu hii changamoto kwetu na Wilaya hii inafursa nyingi ya kuzitangaza na tunaamini kuwa TBC wanawza kushirikiana nasi katika kufanikisha hili,”alisema Mhe.Lugangika.

[caption id="attachment_39294" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akiwashauri viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Lushoto kuuendeleza uwanja wa michezo wa Sabasaba kwa kuomba wataalamu Wizarani wa kuwapa ushauri wa kiutalamu wa namna ya kuboresha uwanja huo alipotembea uwanja huo leo,wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilayani Lushoto Bw.Amiri Shekelata .[/caption]

Kwa upande wa Meneja wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Bw.Gerald Uisso  alieleza kuwa amapokea maelekezo yote na ofisi yake itahakikisha inazingatia ushauri na kufanikisha zoezi hilo la kuboresha usikivu mapema.

Pamoja na hayo nae Mwenyekiti wa Chama cha CCM Wilaya ya Lushoto alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa chama hicho kimeanzakutafuta mwekezaja wa kuendeleza uwanja wa michezo wa Sabasaba ilikuweza kuuweka katika hali nzuri itakayo faa kwa kutumika katika michezo mbalimbali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi