Serikali imetangaza mikakati madhubuti ya kuhakikisha Tanzania inakuwa mwenyeji bora wa mashindano ya 74 ya Miss World yatakayofanyika mwaka 2027, kufuatia kusainiwa kwa mkataba rasmi wa maandalizi hayo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda amesema maandalizi ya mashindano hayo yatazingatia viwango vya kimataifa, huku yakilenga kuleta manufaa mapana kwa taifa.

Mhe. Makonda amesema serikali imejipanga kutumia tukio hilo kama chachu ya kukuza sekta ya utalii, kuongeza mapato ya ndani na kufungua fursa mpya za ajira kwa vijana, hususan katika sekta za hoteli, usafiri na burudani.
“Tunatarajia kupokea zaidi ya wageni 20,000 kutoka mataifa mbalimbali, huku takribani watazamaji bilioni mbili duniani wakifuatilia kupitia televisheni na mitandao ya kijamii. Hii ni fursa kubwa ya kuitangaza Tanzania kimataifa,” amesisitiza Makonda.
Ameongeza kuwa mafanikio hayo yanatokana na juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kufungua milango ya kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia Diplomasia ya Utalii na Utamaduni akibainisha kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa ndani na kimataifa ili kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa ufanisi na kwa wakati, sambamba na kuimarisha miundombinu muhimu itakayohitajika wakati wa mashindano hayo.

Mhe. Makonda ameeleza kuwa tukio hilo litakuwa jukwaa muhimu la kuitangaza Tanzania duniani, hasa katika vivutio vya utalii, utamaduni na urithi wa taifa, hatua itakayosaidia kuongeza idadi ya watalii wanaoitembelea nchi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema ujio wa mashindano ya Miss World utawafungulia fursa mabinti wa Kitanzania kushiriki na kunufaika kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali zitakazoambatana na tukio hilo.
Ameongeza kuwa dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza sekta ya sanaa na utamaduni imechangia kwa kiasi kikubwa Tanzania kupata fursa hiyo ya kihistoria ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa dunia