Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Yafikia Lengo Uwekaji Anwani za Makazi-Nape
May 20, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mawazo Kibamba, MAELEZO

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) amesema hadi kufikia tarehe Aprili 30, 2022 jumla ya anwani za makazi 12,171,320 zimekusanywa na kuingizwa kwenye Programu tumizi ikiwa ni sawa na asilimia 104.3 ya lengo la jumla ya Anwani 11,676,891 zilizopangwa kukusanywa katika Mikoa yote nchini.

Ameyasema hayo leo Mei 20, 2022 Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2022/2023 ya Wizara hiyo.

Nape amesema kufuatia malengo ya Serikali ya kukamilisha Anwani za Makazi kabla ya Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwezi Agosti, 2022, katika Kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa kilichofanyika tarehe 08 Februari, 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alielekeza Mfumo wa Anwani za Makazi kutekelezwa kwa Mfumo wa Operesheni, aliyoipa jina la “OPERESHENI ANWANI ZA MAKAZI”.

“Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI zimeendelea na utekelezaji wa Mradi chini uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, amesema Mhe. Nape.

Amesema katika mwaka wa fedha 2021/22 shughuli nyingine zilizotekelezwa ni pamoja na kuunda programu tumizi (Mobile application) ya mfumo iliyoongeza ufanisi katika matumizi na utekelezaji wa mfumo na kuongeza kuwa programu hiyo imetumika katika kukusanya taarifa za barabara, mitaa, njia, makazi na wakazi sambamba na kumuongoza mtu kutoka anwani ya makazi moja kwenda anwani ya makazi nyingine.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi