Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Yaanza Mpango wa Kurejesha Mali Kale Zilizo Nje ya Nchi
Jan 30, 2024
Tanzania Yaanza Mpango wa Kurejesha Mali Kale Zilizo Nje ya Nchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samweli Shelukindo akizungumza na Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu kuhusu kuandaa Mpango wa kurejesha mali kale mbalimbali zilizopo nje ya nchi ambazo zilichukuliwa wakati na baada ya Utawala wa Kikoloni
Na Shamimu Nyaki

Serikali ya Tanzania imeanza kuandaa Mpango wa kurejesha mali kale mbalimbali zilizopo nje ya nchi ambazo zilichukuliwa wakati na baada ya Utawala wa Kikoloni kwa lengo la kuhifadhi, Kulinda na kuenzi historia na utamaduni wa Tanzania.

Mpango huo umeanza kutekelezwa kupitia Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu inayoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samweli Shelukindo, ambapo Januari 30, 2024 jijini Dodoma viongozi hao wamekutana kujadili namna ya kutekeleza mpango wa urejeshwaji huo.

Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine kimebainisha kuwa upo umuhimu wa kurejesha mali kale hizo ili kurejesha heshima na utu, kukuza utalii wa ndani na nje, kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Mataifa mengine, Utambulisho wa Taifa pamoja na kuongeza pato la Taifa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi