Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania ni Jamhuri ya Wapambanaji, Bado nafasi tunayo: Mhe.Gekul
Oct 13, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Shamimu Nyaki- Goa, India

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul, ameendelea kuwatia hamasa na moyo Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Girls’ inayoshiriki Kombe la Dunia nchini India.

Akizungumza na timu hiyo mara baada ya mchezo uliochezwa Oktoba 12, 2022 uliomalizika kwa Japan kuifunga Tanzania Magoli 4 - 0 kutokana  na Tanzania kupata kadi nyekundu mapema katika kipindi cha kwanza, amesema nafasi ya kufanya vizuri bado ipo katika mechi mbili zijazo.

"Watoto wetu wanauwezo, wameonesha mpira wa kiwango kikubwa sana, wamekua na ari muda wote wa mchezo, zaidi nampongeza Golikipa Zuhura kwa kuokoa magoli mengi yaliyoelekezwa golini kwetu," amesema Mhe. Gekul.

Ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kuiunga mkono timu hiyo na kuwekeza zaidi na zaidi katika vipaji kuanzia umri mdogo.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisia Mbega amesema kwa kipindi chote timu itakayokua nchini India itahakikisha mazingira na maandalizi ya michezo mingine ijayo yanakua bora.

Serengeti Girls sasa inajiandaa kukabiliana na Ufaransa Oktoba 15, 2022.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi