Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TANZANIA NCHI YA KWANZA KUWA NA RELI YA KISASA YA MASAFA MAREFU AFRIKA
Apr 12, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_274" align="aligncenter" width="629"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Pugu Stesheni kwa ajili ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) kutoka Dar hadi Morogoro yenye urefu wa Kilomita 300 katika hafla iliyofanyika Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.[/caption] [caption id="attachment_277" align="aligncenter" width="720"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa Kilomita 300 katika hafla iliyofanyika Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.[/caption] [caption id="attachment_278" align="aligncenter" width="630"] Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa Kilomita 300 katika hafla iliyofanyika Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.[/caption] [caption id="attachment_279" align="aligncenter" width="629"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akielekea katika eneo lililotengwa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya hafla ya uwekaji wa jiwe hilo katika mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa Kilomita 300, hafla iliyofanyika Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.[/caption] [caption id="attachment_280" align="aligncenter" width="629"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akifutilia maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa Reli ya Kati wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi huu kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_283" align="aligncenter" width="720"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akionyesha zawadi ya mchoro wa Reli wakati hafla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Reli ya Kati yenye Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) leo jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_284" align="aligncenter" width="629"] Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_286" align="aligncenter" width="629"] Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_287" align="aligncenter" width="629"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akiwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Reli ya Kati ya yenye Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) leo jijini Dar es Salaam[/caption]

Picha na Frank Shija

Na. Immaculate Makilika

Tanzania inatarajiwa kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na reli ya kisasa inayotumia umeme na mafuta itakayokuwa na uwezo wa kusafiri  masafa marefu kwa mwendokasi wa kilometa 160 kwa saa. Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msingi wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli hiyo ya leo huko Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa reli hiyo itakuwa ya kisasa zaidi barani Afrika na itasaidia kukuza uchumi wa nchi kwa kuchochea fursa za biashara ndani na nje ya nchi. Awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli hiyo ambayo itahusisha kipande cha kilomita 300 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro utagharimu jumla ya shilingi trilioni 2.8 na utatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 30. Dkt Magufuli alitoa mfano wa nchi zenye reli za mwendokasi lakini masafa mafupi barani Afrika kuwa ni Morocco ambayo inasafiri kwa mwendokasi wa kilomita 220 kwa saa na Afrika Kusini inayosafiri mwendokasi 150 kwa saa. Dkt Magufuli alieleza kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na treni itakayosafiri masafa marefu kwa mwendokasi wa km 160 kwa saa. Alifananua kuwa mradi huo wa ujenzi wa reli unatekelezwa kwa fedha za Tanzania ambapo tayari serikali imeshawalipa wakandarasi malipo ya awamu ya jumla ya shilingi bilioni 300. Akizungumzia umuhimu wa ujenzi wa reli hiyo, Rais Magufuli alisema kuwa reli hiyo itasaidia kuongeza kasi ya usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam kwa haraka na kuwafikia wateja ndani ya muda mfupi. Vilevile, reli hiyo itarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo pamoja na kukuza biashara kati ya Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudani ya Kusini. Sambamba na hayo, Rais Magufuli alisema kuwa ujenzi wa reli hiyo utasaidia kuimarisha sekta nyingine za uchumi ikiwemo utalii, viwanda, kilimo, pamoja na kutoa ajira kwa watanzania ambapo kutakuwa na ajira muda zipatazo 600,000, na ajira za kudumu 30,000. Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema kuwa reli hiyo ya kisasa inayojengwa na wakandarasi kutoka muungano  wa kampuni mbili za nchi ya Uturuki na Ureno  itakuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo tani 10,000 kwa mara moja  na kutumia saa 2 kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na saa 7 na dakika 40 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza. Naye, Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya ujenzi kutoka Uturuki ya Yapi Merkezi Bw.  Emre Aykar alisema kuwa reli hiyo itaimarisha zaidi uhusiano wa Uturuki na Tanzania na kuongeza kiwango cha shughuli za biashara nchini. “Tunaahidi kujitahidi kumaliza mradi kwa wakati na katika kiwango kinachotakiwa” alisema Bwana Aykar. Reli hiyo ya kisasa inatarajiwa kujengwa pembeni ya reli ya kati ambayo ilijengwa wakati wa utawala wa kikoloni wa Wajerumani na Waingereza miaka 112 iliyopita.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi