Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania na Afrika Kusini za Saini Mikataba Mitatu ya Ushirikiano
May 11, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_814" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbambali yatokanayo na ziara ya Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Jacob Zuma (kulia) Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Rais Zuma yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia jana.Ziara hiyo imefuatia mwaliko maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais Magufuli walipokutana katika kikao cha Umoja wa Afrika(AU) kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.[/caption] [caption id="attachment_817" align="aligncenter" width="630"] Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Jacob Zuma akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu mambo mbambali yatokanayo na ziara yake nchini Tanzania leo Ikulu, Jijini Dar es Salaam. Rais Zuma yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia jana ambapo amekutana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) na kujadiliana mambo kadhaa kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari.[/caption] [caption id="attachment_820" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Jacob Zuma (kushoto) mara baada ya kumpokea katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Rais Zuma yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais Magufuli walipokutana katika kikao cha Umoja wa Afrika(AU) kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.[/caption]     [caption id="attachment_826" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Jacob Zuma akikagua Gwaride la Jeshi la Ulinzi Tanzania (JWTZ) alipopokelewa katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Rais Zuma yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli walipokutana katika kikao cha Umoja wa Afrika(AU) kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.[/caption] [caption id="attachment_827" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Jacob Zuma (kushoto) akiwapunguia mkono wananchi waliofika kumpokea katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Rais Zuma yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais Magufuli walipokutana katika kikao cha Umoja wa Afrika(AU) kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.[/caption] [caption id="attachment_828" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wananchi wakimlaki Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Jacob Zuma (hayupo pichani) wakati alipokuwa akielekea katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Rais Zuma yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais Magufuli walipokutana katika kikao cha Umoja wa Afrika(AU) kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.[/caption] [caption id="attachment_832" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Jacob Zuma (kushoto) akifurahia ngoma kutoka kwa moja ya kikundi kilichoandaliwa kwa ajili ya mapokezi yake, mara baada ya kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Rais Zuma yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais Magufuli walipokutana katika kikao cha Umoja wa Afrika(AU) kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.[/caption] [caption id="attachment_835" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Jacob Zuma (kushoto) akifurahia kupiga ngoma mara baada ya kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Rais Zuma yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais Magufuli walipokutana katika kikao cha Umoja wa Afrika(AU) kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.[/caption] [caption id="attachment_838" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashari Balozi Dkt. Agustine Mahiga akibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano wa Kidiplomasia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Bi. Maite Nkoana – Mashabane iliyotiwa saini na mawaziri hao wakati wa ziara ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma leo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya mikataba mitatu ambayo mingine ni makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya Uchukuzi, na Bio Unuwai na Uhifadhi.[/caption] [caption id="attachment_839" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Waziri wa Mazingira wa Afrika Kusini Bi. Edna Mlowe wakiweka saini katika hati ya makubaliano ya ushirikiano wa Bio unuwai na uhifadhi kati ya Tanzania na Afrika Kusini wakati wa ziara ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Jumla ya mikataba mitatu ambayo mingine ni makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya Diplomasia na Uchukuzi.[/caption] [caption id="attachment_840" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania Mhandisi Edwin Ngonyani akibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya usafirishaji na Waziri wa masuala ya Usafirishaji wa Jamhuri ya Afrika Kusini Makachani Maswanganyi mara baada ya kuweka saini hati hizo wakati wa ziara ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma leo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya mikataba mitatu ambayo mingine ni makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya Diplomasia ya Kimataifa, na Bio Unuwai na Uhifadhi.[/caption] [caption id="attachment_841" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Jacob Zuma (kulia) ya kumaliza mazungumzo yao nao waandishi wa habari leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais Zuma yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais Magufuli walipokutana katika kikao cha Umoja wa Afrika(AU) kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.[/caption] [caption id="attachment_842" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustine Mahiga akiteta jambo na baadhi ya mawaziri kutoka Afrika Kusini mara baada ya kumaliza kwa mazungumza baina ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa Tanzania na Jacob Zuma wa Afrika Kusini hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Waziri wa Mazingira wa Afrika Kusini Bi. Edna Mlowe na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Maite Nkoana – Mashabane. Picha zote na: Frank Shija[/caption] Na. Beatrice Lyimo na Immaculate Makilika Serikali za Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania na Afrika ya Kusini zasaini mikataba mitatu ya ushirikiano katika sekta mbalimbali zitakazosaidia kukuza uchumi wa nchi hizo mbili. Hati za mikataba hiyo  zimesainiwa leo Ikulu Jijini  Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Marais  wawili Dkt. John Magufuli  na  Jacob Zuma  na waandishi wa habari. Mikataba iliyosainiwa baina ya nchi hizo mbili  ni hati ya muhtasari  wa makubaliano ya mkutano wa tume ya pamoja ya Marais kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Afrika Kusini uliolenga kuboresha makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mkutano huo. Hati ya makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya Bi Anuwai kati ya Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini, inayolenga kuboresha ushirikiano katika sekta ya wanyamapori na uhifadhi. Huku hati nyingine ikiwa ni makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya uchukuzi kati ya Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini uliolenga kuboresha ushirikiano katika sekta ya uchukuzi. Akizungumza wakati wa mkutano huo Rais Magufuli alisema ziara ya Rais Zuma imekwenda sambamba na mkutano wa kwanza wa tume ya Marais ambapo ulibainisha baadhi ya maeneo ya makubaliano. Rais Magufuli alisema kuwa maeneo ya makubaliano hayo yalilenga kuimarisha na kukuza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili na njia za kundoa vikwazo vinavyokwamisha biashara baina yao. “Hali ya biashara ya Afrika Kusini nchini kwa mwaka 2016 ni takribani Tsh Trilion 2.4  na uwekezaji wake ni Dola za Kimarekani 803.15 milioni iliyopelekea kupatikana kwa ajira kwa watanzania 20,916”alisema Rais Magufuli Rais Magufuli alitaja maeneo mengine ya makubaliano kuwa ni kushirikiana katika  sekta ya viwanda  ambapo amewakaribisha wafanyabiashara kutoka nchini Afrika Kusini ili kuwekeza  katika kujenga viwanda vya kusindika mazao na hivyo  kukuza uchumi. Kwa upande wa Sekta ya miundombinu na nishati wamelenga katika kuimarisha reli ya kati na upatikanaji wa umeme, ambapo Rais Dkt.Magufuli amemwomba Rais Zuma kutumia ushawishi wake katika Umoja wa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi (BRICS) ili kuisaidia Tanzania kupata mkopo kwa gharama nafuu, kwa lengo la kuendeleza ujenzi wa miradi ya reli ya kati na umeme. Vilevile, Marais hao wamekubaliana kubadilishana uzoefu na wataalamu kupitia sekta ya utalii ikiwemo kuwakiribisha wawekezaji kutoka nchi ya Afrika Kusini kuwekeza  kwa kujenga hoteli za kitalii pembezoni mwa fukwe za bahari ya Hindi. Maeneo mengine ya makubaliano ni pamoja na  sekta za madini kwa kubadilishana uzoefu na utaalamu, afya kwa kuwakaribisha wawekezaji katika ujenzi wa viwanda vya kutengeneza dawa, elimu, sayansi na teknolojia ambapo Rais Zuma amekubali kupokea wataalamu wa lugha ya kiswahili watakaofundisha Afrika Kusini. Rais Zuma alisema wataendelea kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na kukuza umoja wa Afrika ili kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyokabili bara hilo. “Tumefurahi kusaini mikataba hiyo leo, pamoja na kupata taarifa ya mawaziri iliyojitosheleza katika kuainisha maeneo ya ushirikiano na utekelezaji wake itakayosaidia kuleta maendeleo katika nchi hizi mbili” alisema Rais Zuma Rais Jacob Zuma anakamilisha ziara yake ya siku mbili leo usiku iliyolenga  katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili, ikiwa ni pamoja na kuanisha maeneo mapya ya ushirikiano yatakayochochea maendeleo kwa manufaa ya wananchi.      

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi